MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF- AMANI IWE JUU YAKE-07

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF-AMANI IMFIKIE –

Makala namba (7) :

قال تعالى :

Amesema (Allah) aliyetukuka-:

قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ لاَ تَقْتُلُواْ يُوسُفَ وَأَلْقُوهُ فِي غَيَابَةِ الْجُبِّ يَلْتَقِطْهُ بَعْضُ السَّيَّارَةِ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ

Akasema msemaji katika wao : “Msimuue Yusuf ,lakini mtupeni katika kisima kirefu chenye giza ,watamuokota baadhi ya wasafiri ,ikiwa nyinyi (mmeazimia) kulifanya (hilo) .

Maelezo:

Ndugu wa Yusuf -amani iwe juu yake- walipokuwa katika njama juu ya kumtenganisha Yusuf na baba yake wakasema ” ” “muueni” lakini mmoja katika ndugu zake akasema : Musimuue Yusuf…” .
Tena akamtaja kwa jina ili azilainishe nyoyo zao ,kwa maana hata iweje Yusuf ni ndugu yetu ,na wakakubaliana wamtupe ndani ya kisima kirefu chenye kina na chenye giza,ili pindi wasafiri wanaotokea Sham au palestina kuelekea Misr wamuokote ,na huyu aliyetoa rai hii ni yule mwenye mawazo mazuri kuliko wote ,yaani yeye aliona kuwa walifanye lile lenye madhara madogo badala ya kumuua.

Katika hili tunajifunza kuamini qadar ya Allah :Kila kinachotokea kimekadiriwa na Allah ,na kilichokadiriwa na Allah hakuna wa kukizuia mfano hapa kwa sababu Allah -aliyetukuka-alitaka kupitisha jambo lake ambalo hapana budi litokee ambalo ni kumfunulia na kumpa utume Yusuf , na kumpa nguvu na utawala katika nchi ya Misr na kumfanya kuwa ni mfalme kwa ajili hiyo Allah akamuepusha Yusuf na kuuliwa.

Tanbih : Makusudio ya kumtupa Yusuf katika kisima yaani walimtupa pembeni mwa kisima yaani ,zile sehemu zilizoingia ndani kiasi ambacho mtu anaweza kukaa katika jiwe ,haina maana walimtupa kama furushi ndani ya kisima kwa sababu wanajua lau wangefanya hivi wangemuua .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Ramadhani 21, 1442H ≈ May 3, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *