Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
Makala namba (8) :
قَالُواْ يَٰٓأَبَانَا مَالَكَ لَا تَأۡمَ۬نَّا عَلَىٰ يُوسُفَ وَإِنَّا لَهُۥ لَنَٰصِحُونَ (١١)
Wakasema: “Ewe baba yetu una nini hautuamini juu ya Yusuf; Na hakika sisi ni wenye kumfanyia wema ( huruma )?”.
أَرۡسِلۡهُ مَعَنَا غَدٗا يَرۡتَعۡ وَيَلۡعَبۡ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ (١٢)
“Mpeleke kesho pamoja nasi (machungani); atakula kwa furaha na kucheza ;na hakika sisi ni wenye kumlinda “
Maelezo:
Kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo Yaqub – Amani iwe juu yake – kwa mwanaye Yusuf – Amani iwe juu yake – alikuwa hataki kuona anatoweka machoni kwake! na baada ya ndugu wa Yusuf kupanga njama ya kumtenganisha ndugu yao Yusuf na baba yake, na walichukua rai aliyoitoa yule ndugu yao ya kumuweka ndani ya kisima, baada ya hapo walikuja kumuomba baba yao awape Yusuf lakini baba yao aliwakatalia, watoto wakamuuliza baba yao:
“Ewe baba yetu una nini hautuamini juu ya Yusuf; Na hakika sisi ni wenye kumfanyia wema ?”
Na maneno haya ya ndugu wa Yusuf yanajulisha kuwa walishamuomba sana baba yao awape Yusuf lakini hakukubali.
Ndugu wa Yusuf -Amani iwe juu yake – wakamuomba baba yao awape Yusuf ili waende naye machungani akale na kucheza kwa furaha ,kwa hiyo hapa tunajifunza kuwa si vibaya ukijisikia uchovu ,na msongo wa mawazo ukaenda mabustanini ,mashambani pembeni mwa mji , kwa matembezi na kujistarehesha na kuondoa uchovu n.k , na jambo hilo- limehibiti kwa mtume kama alivyosema Aisha-Allah amridhie-baada ya kuulizwa na Shuraih Al-harithiy – :
هل كان النبي صلى الله عليه وسلم يبدو؟ قالت: نعم، كان يبدو إلى هذه التلاع”؛
“Je Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-/alikuwa akienda mashambani /nje ya mji ?akajibu : Ndio ,alikuwa akienda katika hizi sehemu zenye mabonde yenye kutiririka maji ”
رواه أحمد (٢٤٣٠٧)، وأبو داود (٢٤٧٨)، وصحَّحه ابنُ حِبَّان (٥٥٠).
Kwa ajili hii akasema ibn Rajab- Allah amrahamu-:
“أما الخروج إلى البادية أحيانًا للتنزُّه ونحوه في أوقات الربيع وما أشبهه: فقد ورد فيه رخصة”،
“Ama kwenda mashambani (mabustanini) baadhi ya nyakati kwa ajili ya matembezi na mfano wa hayo (matembezi) katika majira ya kipupwe na mfano (majira) hayo (yenye hali ya kuvutia) ,bila shaka kumekuja ruhusa katika hilo (ktk sheria) ”
(فتح الباري 1/ 116).
Kisha akataja hadithi tuliyoitaja hapo juu .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Ramadhani 23, 1442H ≈ May 5, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•