MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF-AMANI IWE JUU YAKE –

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF -AMANI IWE JUU YAKE –

Makala namba (9) :

قال تعالى :

Amesema (Allah) aliyetukuka-:

قَالَ إِنِّي لَيَحۡزُنُنِيٓ أَن تَذۡهَبُواْ بِهِۦ وَأَخَافُ أَن يَأۡكُلَهُ ٱلذِّئۡبُ وَأَنتُمۡ عَنۡهُ غَٰفِلُونَ (١٣)

(Baba yao) akasema : “Kwa hakika linanihuzunisha mimi (hili jambo la) nyinyi kwenda naye (huko) na ninaogopa (asije) mbwa mwitu akamla na hali ya kuwa nyinyi mumeghafilika naye (katika kazi zenu) “

قَالُواْ لَئِنۡ أَكَلَهُ ٱلذِّئۡبُ وَنَحۡنُ عُصۡبَةٌ إِنَّآ إِذٗا لَّخَٰسِرُونَ (١٤)

Wakasema : “Ikiwa mbwa mwitu atamla,na hali ya kuwa sisi ni kundi ,bila shaka tutakuwa ni wenye kupata hasara “

Maeleo :

Kama tulivyoeleza katika tarjama ya aya zilizopita kuwa kutokana na mapenzi makubwa ya Yaqub kwa mwanaye kitendo cha kupotea tu machoni mwake hupatwa na huzuni ! , na watoto walipomuomba baba yao ruhusa ya kuondoka na Yusuf ,baba yao aliwakatalia kwa kuhofia kuwa huwenda wakashughulishwa na michezo na wakamuacha Yusuf peke yake na akaliwa na mbwa mwitu ,huwenda sehemu walizokuwa wakiishi kulikuwa na mbwa mwitu wengi kama walivyoeleza baadhi ya wanachuoni .
Baada ya ndugu wa Yusuf kumtoa wasi wasi na kumtuliza baba yao na kumueleza kuwa wao ni wengi wanauwezo wa kumlinda na kumuhifadhi na kama akiliwa na mbwa mwitu basi huo wingi wao utakuwa si lolote si chochote ,na watakuwa ni wenye kupata hasara ,mwishowe baba yao alikubali na akawaruhusu waondoke na Yusuf ,na haya yote yalitokea kwa kadari ya Allah ili yatokee yale ambayo Allah ameyakadiria yatokee kwa Yusuf .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shawwal (Mfungo mosi) 3, 1442H ≈ May 15, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *