Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF -AMANI IWE JUU YAKE .
Makala namba (10) :
قال تعالى :
Amesema (Allah ) aliyetukuka-:
فَلَمَّا ذَهَبُواْ بِهِۦ وَأَجۡمَعُوٓاْ أَن يَجۡعَلُوهُ فِي غَيَٰبَتِ ٱلۡجُبِّۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمۡرِهِمۡ هَٰذَا وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ { ١٥}
Basi pindi walipomchukua na wakakubaliana kumtia katika kina cha kisima, (walipofanya hivyo). Na tukampa wahyi “Utawaambia jambo lao hili hali wao hawatambui .
Maelezo :
Ina maana baada ya baba yao kuwaruhusu hao ndugu wa Yusuf kwenda na Yusuf -amani iwe juu yake- huko machungani /matembezini ,wakaenda na baada ya kumtupa na kumuweka ndani ya kisima Allah -aliyetukuka- akamfahamisha Yusuf kwa kumtia ilhamu katika moyo wake au ,au kwa kumtuma malaika Jibrir ,kuwa yeye Yusuf atakuja kuwaeleza hao ndugu zake haya waliyomfanyia muda ambao hao ndugu zake watakuwa hawamjui kuwa huyu ni Yusuf -amani iwe juu yake- kwa sababu wao dhana yao kuwa Yusuf ameshakufa !, na hapo ni pale watapokufa hao ndugu zake kuja kutaka chakula kutoka Mashariki ya kati baada ya kupatwa na balaa la njiaa, na walipoingia katika nchi ya Misr na kipindi hicho ilikuwa na hali mzuri na sifa zake zilienea kwa hiyo watu walikuwa wakitoka sehemu mbali mbali ili kupata chakula na walipofika kwa Yusuf , Allah anasema :
{ وَجَاءَ إِخْوَةُ يُوسُفَ فَدَخَلُوا عَلَيْهِ فَعَرَفَهُمْ وَهُمْ لَهُ مُنكِرُونَ }
{ Wakaja ndugu wa Yusuf (kutoka Sham) na wakaingia kwake ; (Yusuf) akawajua ,(lakini) wao hawakumjua } .
سورة يوسف ٥٨ .
Na baada ya hapo katika aya za mbele baada ya kutokea yale yaliyotokea akawaeleza kuwa Yeye ni Yusuf -amani iwe juu yake- na ndugu yake,kama tutakavyojua katika muendelezo ya tarajma yetu – inshaallah .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 11, 1442H ≈ May 23, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•