Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF- AMANI IWE JUU YAKE .
Makala namba (12) :
قال تعالى :
وَجَاءُوا عَلَىٰ قَمِيصِهِ بِدَمٍ كَذِبٍ ۚ قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنْفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ وَاللَّهُ الْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ (١٨)
Amesema (Allah) aliyetukuka-:
“Na wakaja na kanzu yake yenye damu ya uwongo . (Baba yao) akasema :Bali nafsi zenu zimewapambia jambo .Basi subira (yangu ni subira) njema ; na Allah pekee ndiye aombwaye msaada kwa haya mnayoyasema .
سورة يوسف (١٨)
Maelezo ya muandaaji :
Pamoja na kuwa walitumia hila kadhaa ktk kufanikisha jambo lao kama vile kurudi usiku hali ya kuwa wakilia ,lakini pia walirudi na kanzu ya Yusuf hali ya kuwa wameipaka damu !ili kuufanya uwongo wao kuwa ni ukweli ,na hii ni dalili kuwa Yusuf- amani iwe juu yake- alikuwa akivaa kanzu.
Pamoja na hila hizi walizotumia ili kuupamba uwongo wao lakini baba yao alijua kuwa wao ni waongo kutokana na dalili na ishara kama vile ile damu iliyopo katika ile kanzu haikuwa ni damu halisi ya mwanadamu na pia ile kanzu haikuchanika !,lakini pamoja na mtihani huu mkubwa uliompata Yaqub -amani iwe juu yake- aliwaambia wanae kuwa yeye ni mwenye kusubiri juu ya mtihani huu subira iliyokuwa mzuri ,na subira mzuri ni ile ambayo haina malalamiko ndani yake kwa viumbe , kama alivyosema Allah alipomuelezea Yaqub mwishoni mwishoni mwa sura hii :
قَالَ إِنَّمَا أَشْكُو بَثِّي وَحُزْنِي إِلَى اللَّهِ …(٨٦)
Akasema (Yaqub) : Hakika mimi namshtakia Allah sikitiko langu na huzuni yangu .
Suratu Yusuf (86) .
Na pia Yaqub -amani iwe juu yake- akawaeleza wanae kuwa Allah atampa msaada juu ya huo uwongo wanaomuongopea .
Miongoni mwa faida tunazopata katika aya hii kama walivyotaja wanachuoni ni hizi:
1- Husuda hupelekea kumfanyia vitimbi yule anayehusudiwa kama ilivyotokea kwa ndugu wa Yusuf kwa ndugu yao Yusuf .
2- Hasidi hata kama akidai na kudhihirisha kuwa yeye anampenda yule anayemhusudu huwa si mkweli, kama walivyokuwa wakidhihirisha ndugu wa Yusuf kuwa wao wanampenda Yusuf .
3- Yule mwenye kutaka kufanikisha jambo lake kwa kumuasi Allah basi Allah atamfedhehesha !.
4- Tahadhari haimuhifadhi mtu kutokana na makadirio ya Allah .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 20, 1442H ≈ Jun 1, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•