MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF-AMANI IWE JUU YAKE-

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

MAZINGATIO KATIKA
KISA CHA NABII YUSUF -AMANI IWE JUU YAKE-

Makala namba (13) :

قال تعالى :

Amesema (Allah ) -aliyetukuka-:

وَجَآءَتۡ سَيَّارَةٞ فَأَرۡسَلُواْ وَارِدَهُمۡ فَأَدۡلَىٰ دَلۡوَهُۥۖ قَالَ يَٰبُشۡرَىٰ هَٰذَا غُلَٰمٞۚ وَأَسَرُّوهُ بِضَٰعَةٗۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ (١٩)

Ukafika msafara (karibu na kisima) ,wakawatuma wateka maji wao ,na (mmoja wao) akatumbukiza ndoo yake (aliponyanyua ndoo akamuona mtoto) alisema: “Ee (huu ndio mwanzo wa) furaha njema !Huyu hapa kijana mwanamume “.Nao wakamficha (ili wamfanye kuwa ni) bidhaa.Na Allah nimjuzi wa yale waliyokuwa wakiyafanya.

وَشَرَوۡهُ بِثَمَنِۢ بَخۡسٖ دَرَٰهِمَ مَعۡدُودَةٖ وَكَانُواْ فِيهِ مِنَ ٱلزَّٰهِدِينَ (٢٠)
Na wakamuuza kwa thamani duni kwa pesa zenye kuhesabika ,na walikuwa hawana haja naye.

Maelezo ya muandaaji:

Baada ya ndugu wa Yusuf-Amani iwe juu yake – kumuweka ndugu yao Yusuf katika hiki kisima chenye kina kirefu ima waliondoka au walisogea karibu na hapo kama walivyosema wanachuoni wengine.

Na baadaye kukatokea msafara wa wasafiri uliokuwa ukielekea Misr ,na pindi walipohitajia maji wakubwa wa ule msafara wakawatuma baadhi ya watu wao kwenda kutafuta maji ,wakafanikiwa kukiona kisima na pindi mmoja wao alipoingiza ndoo ili kuchota maji na alipoinyanyua hiyo ndoo akamuona mtoto mzuri mwenye kupendeza badala ya kushtuka alifurahi kutokana na uzuri wa huyu mtoto ! , na hawakuwaambia wale wakubwa wao kuwa wamepata mtoto bali walimficha ili pindi watapofika Misr wamfanye kuwa ni bidhaa yaani wamuuze ,au baadhi ya wanachuoni wanasema : Waliomficha Yusuf hapa ni ndugu zake , kwa sababu baada ya kumtupa kisimani walikaa karibu kidogo na kisima , na walipoulizwa kuhusu Yusuf wakasema huyo ni mtumwa .

Na baada hapo hao ndugu wa Yusuf wakamuuza Yusuf kwa thamani duni kwa pesa zinazohesabika ,kwa sababu walikuwa hawana haja naye , au baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa : wale wasafiri walimficha Yusuf na hawakuwaambia wakubwa wao na wakaenda kumuuza walipofika Misr kwa bei duni ili waepukane naye kwa sababu walimuona ni kama mzigo kwao, kwa sababu hakumpata kwa juhudi kubwa.

Na yote haya yanatendeka kwa qadar ya Allah -aliyetukuka- ili Yusuf aje kununuliwa na Waziri mkuu wa misri na baadaye aje kuwa ni kiongozi mkubwa .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 25, 1442H ≈ Jun 6, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *