Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU-AMANI IWE JUU YAKE-
Makala namba (21) .
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka-:
فَلَمَّا سَمِعَتْ بِمَكْرِهِنَّ أَرْسَلَتْ إِلَيْهِنَّ وَأَعْتَدَتْ لَهُنَّ مُتَّكَأً وَآتَتْ كُلَّ وَاحِدَةٍ مِّنْهُنَّ سِكِّينًا وَقَالَتِ اخْرُجْ عَلَيْهِنَّ فَلَمَّا رَأَيْنَهُ أَكْبَرْنَهُ وَقَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ وَقُلْنَ حَاشَ لِلَّهِ مَا هَذَا بَشَرًا إِنْ هَذَا إِلاَّ مَلَكٌ كَرِيمٌ ( ٣١)
Basi (mke wa waziri) aliposikia vitimbi vyao (hao wanawake) aliwaita na akawafanyia karamu na akampa kila mmoja katika wao kisu na akamwambia (Yusufu), “Tokeza mbele yao”.Basi walipomuona waliona ni kitu kikubwa kabisa na wakakata mikono yao (bila ya kujijua) na wakasema: ”Hasha lillah! Huyu si mwanadamu ; hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu”.
قَالَتْ فَذَلِكُنَّ الَّذِي لُمْتُنَّنِي فِيهِ وَلَقَدْ رَاوَدتُّهُ عَن نَّفْسِهِ فَاسْتَعْصَمَ وَلَئِن لَّمْ يَفْعَلْ مَا آمُرُهُ لَيُسْجَنَنَّ وَلَيَكُونًا مِّنَ الصَّاغِرِينَ (٣٢)
(Mke wa waziri) akasema : Huyu ndiye mliyenilaumia ; hakika nilimtaka kinyume cha nafsi yake ,lakini akajilinda .Na kama hatafanya ninalomuamrisha ,bila shaka atafungwa gerezani na atakuwa miongoni mwa madhalili.
Maelezo ya muandaji:
Na yule mke wa waziri pindi alipojua kuwa hawa wanawake wamezungumza maneno hayo kwa vitimbi ,na yeye alikuwa na vitimbi zaidi kuliko wao basi akawaita hao wanawake ili waje waone uzuri wa Yusufu wajue kuwa yeye kumpenda Yusufu hana lawama ,na akawaandalia karamu na akawawekea matakia na mito ya kuegemea na akampa kila mmoja wao kisu , na akamuamrisha Yusufu atoke basi wale wanawake walipomuona wakaona ni jambo kubwa ni uzuri wa kushangaza mpaka wakawa wanaikata mikono yao bila ya kuhisi, walishindwa kusubiri na kuvumilia na walirukwa na akili kwa kuona uzuri wa Yusufu na wakamtakasa Allah na wakasema: Huyu si mwanadamu ; hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu”.
Na Yusufu -Amani iwe juu yake- alipewa nusu ya uzuri kama alivyosema Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- pindi alipoenda safari ya Miraji alimuona Yusuf katika mbingu ya tatu akamuelezea kama ifuatavyo:
فَإِذَا أَنَا بِيُوسُفَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِذَا هُوَ قَد اُعْطِيَ شَطْرَ الْحُسْنِ….
“..Basi ghafla nikawa na Yusufu -swala na salamu za Allah zimfikie- ,ghafla (nikamuona) bila shaka amepewa nusu ya uzuri ”
رواه مسلم ١٦٢ .
Ina maana uzuri umegawanywa sehemu mbili nusu (moja) amepewa Yusufu na nusu (nyingine) imegawanywa kwa viumbe wengine .
Kisha baada ya wale wanawake kumuona Yusufu ,yule mke wa waziri akaweka wazi maneno yake akasema kuwa huyu ndiye ambaye mumenilaumu kwa ajili yake, na akaeleza kuwa yeye alimtaka Yusufu lakini Yusufu alijizuia ,na hapa utaona kuwa maneno ya huyu mwanamke yanajulisha kuwa yeye mwenyewe anakubali kuwa Yusufu ametwaharika kwa maana ni msafi wa moyo na msafi wa maumbile na ametakasika na hayo anayomuhitajia .
Na huyu mwanamke akamtisha Yusufu mbele ya hawa wanawake kwa kusema kuwa kama hatofanya lile nililomuamrisha nitamfunga na atakuwa katika madhalili ,kwa maana ana uwezo wa kumfunga kwa sababu ya nafasi aliyokuwa nayo na vilevile anaweza akawa katika madhalili .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 4, 1443H ≈ September 11, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•