https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU -AMANI IWE JUU YAKE-
Makala namba (14) :
قَالَ تَعَالَى :
Amesema (Allah) aliyetukuka-:
{{ وَقَالَ الَّذِي اشْتَرَاهُ مِنْ مِصْرَ لِامْرَأَتِهِ أَكْرِمِي مَثْوَاهُ عَسَىٰ أَنْ يَنْفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا ۚ وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي الْأَرْضِ وَلِنُعَلِّمَهُ مِنْ تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَىٰ أَمْرِهِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ }}
{{ Na yule aliyemnunua huko Misri alimwambia mke wake :
“Ishi nae kwa wema (mtumwa) huyu ;huenda akatufaa (katika kututumikia) au tukampanga kuwa mtoto”. Na kama hivyo tulimmakinisha (tulimkalisha)Yusuf katika nchi (ya Misri) ili kumfundisha tafsiri ya ndoto .Na Allah ndiye Mwenye kushinda juu ya jambo lake ;lakini watu wengi hawajui .}}
يوسف ٢١
Maelezo ya muandaaji:
Ule msafara ulipofika Misri ulimuuza Yusufu kwa mtu mkubwa na mwenye nafasi katika serikali ya Misri inasemekana ima alikuwa ni waziri mkuu au nafasi nyinge katika serikali , na yule waziri mkuu pindi alipomnunua Yusufu akamuamrisha mkewe aishi naye vizuri na amfanye kuwa ni mwenye nafasi, na akataraji kuwa baadaye atawafaa katika huduma mbalimbali ,au watamfanya kuwa ni mtoto kwa sababu wao hawana mtoto , na huyu waziri alikuwa na uoni wa mbele ( فِراسة) kwa sababu pindi alipomuona tu Yusufu kana kwamba alijua nafasi atakayokuwa nayo Yusufu -Amani iwe juu yake- , akamwambia mkewe maneno hayo.
Vilevile kama Allah alivyomuokoa Yusufu kutokana na kifo ,na akamuokoa kisimani baada ya hapo akammakinisha Yusufu na akawa na nafasi kubwa katika serikali ya Misri ,na Allah amelifanya hivi ili amfundishe elimu ya tafsiri ya ndoto na hadithi ya vitabu vingine vya Allah, kitendo cha Allah kumpa nafasi ktk nchi baadhi ya wanachuoni wanasema hili linajulisha kuwa mwenye kujishughulisha na elimu anahitaji awe na wasaa katika dunia yaani awe amekunjuliwa kiasi ili aweze kutafuta elimu na kuisambaza .
Jambo la Allah ni lenye kupita na hakuna yeyote mwenye uwezo wa kuzuia ,na katika mambo hayo ni jambo lake ni kumuhifadhi Yusufu na kumchunga pamoja na kuwa ndugu zake walitaka kumuua .
Watu wengi hawajui utukufu na ukubwa wa Allah ,hawajui kuwa chochote anachokikadiria Allah ni lazima kitokee, hawajui kuwa Allah -aliyetukuka- ni muweza juu ya kila kitu.
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 6, 1442H ≈ June 6, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•