MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU-AMANI IWE JUU YAKE- (18)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU -AMANI IWE JUU YAKE- .

Makala namba (18) .

قال تعالى :

Amesema (Allah) aliyetukuka-:

قَالَ هِيَ رَاوَدَتْنِي عَنْ نَفْسِي وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِنْ أَهْلِهَا إِنْ كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِنْ قُبُلٍ فَصَدَقَتْ وَهُوَ مِنَ الْكَاذِبِينَ (٢٦)

(Yusufu) akasema : “Huyo (mwanamke) ndiye aliyenitaka mimi”. Na shahidi /hakimu aliyekuwa katika jamaa wa huyo (mwanamke) akatoa ushahidi (akasema): Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele basi (mwanamke huyo) amesema kweli ,naye (Yusufu) ni katika waongo “.

وَإِنْ كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِنْ دُبُرٍ فَكَذَبَتْ وَهُوَ مِنَ الصَّادِقِينَ (٢٧)

Na kama kanzu yake imechanwa nyuma,basi (mwanamke huyo) amesema uwongo ,naye (Yusufu) ni katika waongo “.

Maelezo ya muandaaji:

Baada ya kutokea yale yaliyotokea na yule mwanamke akatengeneza uongo kuwa Yusuf alikuwa akitaka kumfanyia machafu ,Yusufu naye akajitetea .

Faida tunazozipata sehemu hii ni hizi:

Inatakiwa mtu ajiweke mbali na maeneo yenye shub’ha /utata sehemu ambayo unaweza ukatuhumiwa tuhuma mbaya ,na ndiyo maana Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie -amesema:

، فَمَنِ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ فَقَدِ اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ، وعِرْضِهِ،

” Basi yule aliyejiepusha na shub’ha/ utata bila shaka (atakuwa) ameitakasa dini yake na heshima yake ” .

رواه البخاري ومسلم .

Kuna siku Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- alikuwa amesima na mkewe Swafiyyah -Allah amridhie- wakati wa usiku kipindi ambacho Mtume- swala na salamu zimfikie- alikuwa yupo katika itikafu huyu mkewe alikuwa amemtembelea ,basi Mtume alipokuwa amesimama na mkewe ghafla wakapita watu wawili katika wenyeji wa Madina ,wakatoa salamu na wakaongeza mwendo,basi Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- akawaambi:

على رِسْلِكُما إنها صفيةُ بنتُ حُييّ .

Punguzeni mwendo ,hakika huyu (niliyesimama naye) ni Swafiyyah bint Huyayy

قالا : سبحان الله يا رسولَ اللهِ ! !

(Wale watu) wakasema: Utakasifu ni wa Allah ,ewe Mtume wa Allah (vipi tukutuhumu)!!

قال : إنَّ الشيطانَ يجري منَ الإنسانِ مجرى الدمِ، فخشيتُ أن يقذفَ في قلوبِكما شيئًا – أو قال : شرًّا –

(Mtume) akasema: Bila shaka Shetani hupita kwa mwanadanu katika mapito ya damu ,basi mimi nikachelea atatupia katika nyoyo zenu kitu (chochote) -au alisema- shari.

رواه أبو داود .

Hapa tunaona Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- aliwaita hawa watu kwa kuchelea kuwa huwenda shetani akaingiza kitu katika nyoyo zao na wakamdhania Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- vibaya na ikawa ndiyo sababu ya kuangamia kwao, kwa hiyo ukijiona upo katika hali ambayo watu watakudhania vibaya basi lifanye lile ambalo litawaondoa watu wasiwasi ili wasikudhanie dhana mbaya.

Tanbih: Ama Nabii Yusufu-Amani iwe juu yake- hapa yeye hukujiingiza katika sehemu yenye shub’ha/ utata kwa sababu yeye ni mtumishi wa mule mule ndani kwa yule Waziri mkuu ,kwa hiyo hapa pia tunajifundisha kuwa kama umevunjiwa heshima au ukatuhumiwa basi una haki ya kujitetea.

Vile vile faida tunayoipata hapa ni subira ya Mtume Yusuf kwa kujiepusha na machafu kwa sababu huyu mwanamke alimtaka mara nyingi mno na si mara moja wala mara mbili, ndiyo maana hapa limetumika neno :

مُرَاوَدَةٌ .

Makusudio ya shahidi hapa ni hakimu ,na hakimu ameitwa shahidi hapa ni kwa sababu hukumu inathibiti kwa ushahidi .

Na makusudio ya Shahidi/hakimu aliyehukumu hapa kuna baadhi ya wanachuoni wanasema hafahamiki Allah ndiye ajuae ,na wengine wanasema ni mtoto mdogo ni katika wale watoto wadogo wanne waliozungumza hali ya kuwa wapo katika mbeleko kama ilivyokuja katika hadithi ambayo baadhi ya wanachuoni wanaisahihisha.

Hapa pia tunajifundisha kuwa hakimu huhukumu kwa kutumia ishara na alama kama hapa alivyohukumu kwa kutumia alama ya kuchanika ya kanzu ya Yusufu .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Muharram/Mfungo nne 29, 1443H ≈ September 6, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *