MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU- AMANI IWE JUU YAKE- (19)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU-AMANI IWE JUU YAKE- .

Makala namba (19) .

قال تعالى :

Amesema (Allah) aliyetukuka:

فَلَمَّا رَأَى قَمِيصَهُ قُدَّ مِنْ دُبُرٍ قَالَ إِنَّهُ مِنْ كَيْدِكُنَّ إِنَّ كَيْدَكُنَّ عَظِيمٌ (٢٨)
Basi (mumewe) alipoona kanzu yake imechanwa kwa nyuma akasema: “Hakika hivi ni katika vitimbi vyenu wanawake ;bila shaka vitimbi vyenu ni vikubwa.”

يُوسُفُ أَعْرِضْ عَنْ هَذَا وَاسْتَغْفِرِي لِذَنْبِكِ إِنَّكِ كُنْتِ مِنَ الْخَاطِئِينَ (٢٩)

“ Yusufu! Yaachilie mbali haya .Na wewe (mwanamke) omba msamaha kwa dhambi zako .Hakika wewe ni katika wenye kufanya makosa ”

Maelezo ya muandaaji:

Basi yule waziri mkuu alipojua kuwa mkewe ndiye muongo na yeye ndiye aliyeazimia mabaya na akamsingizia Yusufu, kwa sababu ya kumpenda kwake mkewe mapenzi makubwa mpaka akawa hana nguvu juu yake akasema kwa kumwambia mkewe:

“Hakika hivi ni katika vitimbi vyenu” ,na wala hakusema : Hakika hivi ni katika vitimbi vyako” ,bali alisema : Hakika hivi ni katika vitimbi vyenu”, yaani wanawake wote ili asimsifu mkewe pekee kwa sifa hiyo ya vitimbi /hila .

Na vile vile kwa mapenzi yake kwa mkewe hakumsema sana bali alitosheka kwa kumwambia Yusufu:

“Yusufu !Yaachilie mbali haya.” yaani asiyasimulie ili habari zisienee .

Kwa maana huyu mwanamume alikuwa hajiwezi kwa mkewe au hakuwa na wivu kwa mkewe jambo ambalo halitakikani kwa mume kwa mkewe bali mume anatakiwa awe na wivu kwa mkewe sawa sawa akimuona mkewe anataka kufanya machafu na yeye ni kichocheo kama alivyokuwa huyu mwanamke au akitaka kufanyiwa machafu.

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Muharram/Mfungo nne 30, 1443H ≈ September 7, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *