Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU- AMANI IWE JUU YAKE-
Makala namba : (20)
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka-:
وَقَالَ نِسْوَةٌ فِي الْمَدِينَةِ امْرَأَةُ الْعَزِيزِ تُرَاوِدُ فَتَاهَا عَن نَّفْسِهِ قَدْ شَغَفَهَا حُبًّا إِنَّا لَنَرَاهَا فِي ضَلالٍ مُّبِينٍ (٣٠) .
Na wanawake wa mji ule wakasema: “Mkewe waziri mkuu anamtaka mtumishi wake .Bila shaka yameingia mapenzi ndani ya moyo (wake) . Bila shaka sisi tunamuona yumo katika upotevu ulio wazi ”
Maelezo ya muandaaji:
Pamoja na kuwa Waziri alimwambia Yusufu- amani iwe juu yake- asisimulie habari za lile tukio, lakini habari zilienea katika mji mpaka wanawake wakazungumza kuwa: Mke wa waziri anamtaka mtumishi wake ,na hawa wanawake walizungumza maneno haya si kwa lengo la kupinga kitendo alichokifanya huyu mwanamke isipokuwa walizungumza maneno haya kwa vitimbi ili huyu mke wa Waziri awaoneshe huyo kijana ambaye yeye anamtaka huyo mke wa Waziri mpaka akafitinika naye, tena hawa wanawake katika vitimbi walivyovifanya katika mazungumzo yao walionesha kuwa hilo jambo la huyo mke wa Waziri kumtaka mtumishi wake ni jambo la ajabu lakini lengo lao si hilo :
”Mke wa Waziri anamtaka mtumishi wake”
kisha wakayatia nguvu maneno yao kwa kusema :
“Hakika yamemuingia mapenzi ndani ya moyo (wake) ” .
Kisha hawakotosheka na maneno haya bali waliyatia nguvu maneno yao kwa kusema :
”Bila shaka sisi tunamuona yumo katika upotevu ulio wazi” .
Yote haya waliyazungumza kwa vitimbi ili yule mke wa waziri awaoneshe huyo kijana kama tulivyoeleza hapo juu .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 2, 1443H ≈ September 9, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•