Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU -AMANI IWE JUU YAKE- .
Makala namba (22)
قَالَ رَبِّ السِّجْنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدْعُونَنِي إِلَيْهِ وَإِلاَّ تَصْرِفْ عَنِّي كَيْدَهُنَّ أَصْبُ إِلَيْهِنَّ وَأَكُن مِّنَ الْجَاهِلِينَ
(Yusufu) akasema: “Ee Mola wangu! Nastahabu/napendelea zaidi gereza kuliko haya wanayoniitia; na usiponiondolea vitimbi vyao nitawaelekea na nitakuwa miongoni mwa wajinga(wafanyao maasi)” (33)
فَاسْتَجَابَ لَهُ رَبُّهُ فَصَرَفَ عَنْهُ كَيْدَهُنَّ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
Basi Mola wake mlezi akajibu maombi (dua) yake na akamuondolea vitimbi vyao .Bila shaka yeye ndiye anayesikia na ndiye anayejua . (34)
Maelezo ya muandaaji:
Yusufu alipoona ule mkusanyiko wa wanawake na yale waliyoyafanya akamuelekea Allah kwa kusema “Ee Mola wangu Nastahabu zaidi gereza kuliko haya wanayoniitia” , na hapa Yusufu amewataja hawa wanawake wote kwa maana hawa wanawake wote walimuafiki mke wa waziri walikuwa wakimtaka Yusufu amkubalie lile analolitaka.
Yusufu -amani iwe juu yake- alimwelekea Allah akasema ni bora gereza kuliko haya wanayomuitia na kitendo cha Yusufu kumuelekea Allah -aliyetukuka- hii dalili kuwa yeye ni kiumbe ndiyo maana akaichelea nafsi yake .
Na Allah -aliyetukuka- akajibu maombi hapo hapo , na hapa Yusufu ametukia jina “ربِّ” yaani Mola wangu Mlezi, kwa sababu yeye Allah ndiye Mlezi wake ,na ndiye anayemuhifadhi, na ndiye anayesimamia mambo yake, na ndiye anayempa kile anachokihitaji.
Maana ya kauli yake :
{Bila shaka yeye ndiye anayesikia na ndiye anayejua}
Maana yake : Allah ni mwenye kusikia dua yake Yusufu ,na ndiye anajua hali yake Yusufu na hali za hao wanawake ,na vile vile Allah ni mwenye kusikia yale waliyoyazungumza hawa wanawake.
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 5, 1443H ≈ September 12, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•