MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU -AMANI IWE JUU YAKE –

Makala namba (28)

قال الله تعالى عن يوسف -عليه السلام -:

Amesema Allah aliyetukuka kuhusu Yusufu -amani iwe juu yake -:

{ وَقَالَ لِلَّذِي ظَنَّ أَنَّهُ نَاجٍ مِّنْهُمَا اذْكُرْنِي عِندَ رَبِّكَ فَأَنسَاهُ الشَّيْطَانُ ذِكْرَ رَبِّهِ فَلَبِثَ فِي السِّجْنِ بِضْعَ سِنِينَ }

Na (Yusufu) akamwambia yule aliyejua ya kwamba ataokoka katika wale wawili: “Nikumbuke (nitaje) kwa bwana wako ” .Lakini Shetani alimsahaulisha kumkumbusha bwana wake.Basi (Yusufu) akakaa gerezani miaka kadhaa.

سورة يوسف ٤٢

Maelezo ya mfasiri :

Yusufu -amani iwe juu yake- akamwabia yule aliyejua kuwa ataokoka kutokana na kuawa, naye ni yule aliyeota akikamua mvinyo :

Nitaje kwa Mfalme hali yangu na haya yaliyonitokea,na kisa changu .Huenda akanitoa gerezani! Shetani alimshughulisha akamsahaulisha kumtaja Yusufu kwa Mfalme. Basi Yusufu akabaki gerezani miaka kadhaa na wengi katika wafasiri wanasema Alikaa miaka saba (7) .

Faida tunayoipata hapa ni mtu anatakiwa awe na adabu na Allah katika matamko yake, kama vile alivyosema Allah pindi alipomuelezea yule mtu hakusema kuwa “Alimsahaulisha Allah ” bali alisema :

فَأَنسَاهُ الشَّيْطَانُ ذِكْرَ رَبِّهِ }

” Lakini Shetani alimsahaulisha kumkumbusha bwana wake.

سورة يوسف ٤٢

Na vilevile Allah-aliyetukuka -amesema katika suratul -Kahf kuhusu yule Kijana wa nabii Musa -amani iwe juu yake -:

{ وَمَآ أَنسَىٰنِيهُ إِلَّا ٱلشَّيْطَٰنُ أَنْ أَذْكُرَهُۥ ۚ }
Na hakuna aliyenisahaulisha isipokuwa Shetani.

سورة الكهف ٦٣

Vilevile hapa hakusema kuwa amemsahaulisha Allah -aliyetukuka – ,kwa maana mtu anatakiwa achunge adabu katika matamko yake upande wa Allah ,pamoja na kwamba kila kinachotokea kimekadiriwa na Allah lakini shari haiegemezewi kwake kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – :

وَالشَّرُّ ليسَ إلَيْكَ،

“Na shari hairudi kwako (ewe Allah) ” .

Na vilevile tunaona pale Allah -aliyetukuka -alipowaelezea Majini waliposema :

وَأَنَّا لَا نَدْرِىٓ أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِى ٱلْأَرْضِ أَمْ أَرَادَ بِهِمْ رَبُّهُمْ رَشَدً

Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale waliopo ardhini au Mola wao Mlezi anawatakia uwongofu (kheri).

سورة الجن ١٠

Vilevile hapa hawa Majini pindi walipotaja shari hawakuigemezesha kwa Allah kwa adabu waliyokuwa nayo na pindi walipotaja uongofu na kheri wakaugemezesha kwa Allah.

Muislamu unatakiwa ujue kuwa kila anachokikadiria Allah ni kheri kwa sababu ima kinaweza kikawa ni fadhila au uadilifu :

Mfano neema mbalimbali zinazowafikia waja hizo ni fadhila zake Allah, na adhabu ambazo huwaadhibu wale wanaostahiki kuadhibiwa huo ni uadilifu wake Allah na uadilifu ni kheri.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tatu 15, 1443H ≈ Jul 14, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *