Makala namba (29) :
قال الله تعالى عن الملك :
Amesema Allah aliyetukuka kuhusu mfalme :
وَقَالَ ٱلْمَلِكُ إِنِّىٓ أَرَىٰ سَبْعَ بَقَرَٰتٍۢ سِمَانٍۢ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعَ سُنۢبُلَٰتٍ خُضْرٍۢ وَأُخَرَ يَابِسَٰتٍۢ ۖ يَٰٓأَيُّهَا ٱلْمَلَأُ أَفْتُونِى فِى رُءْيَٰىَ إِن كُنتُمْ لِلرُّءْيَا تَعْبُرُونَ {٤٣}
Na (siku moja) mfalme alisema : “Hakika mimi nimeota ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda.Na nimeona mashuke saba mabichi na mengine yaliyokauka. Enyi waheshimiwa! Niambieni maana ya ndoto yangu, ikiwa nyinyi mnaweza kuagua ndoto.
قَالُوٓاْ أَضْغَٰثُ أَحْلَٰمٍۢ ۖ وَمَا نَحْنُ بِتَأْوِيلِ ٱلْأَحْلَٰمِ بِعَٰلِمِينَ {٤٤}
Wakasema : Ni ndoto zilizoparaganyika , wala sisi sio wenye kujua tafsiri ya ndoto hizi .
Maelezo ya mfasiri :
Allah anaelezea namna faraja ilivyomfikia nabii Yusufu -amani iwe juu yake- na hii faraja inatoka kwa Allah kwa ndoto ambayo alimuonesha mfalme na wala faraja hii haikutokana na yule aliyetoka gerezani.
Mfalme aliota ndoto akakusanya kikundi chake na watu wake maalumu akasema : Nimeota usingizini kuna ng’ombe saba wanene wanaliwa na wengine Saba madhaifu. Na nimeota mashuke saba mabichi, na mengine saba yaliyokauka. Enyi wakubwa, wanazuoni wenye maarifa! Nitoleeni fatwa ya hizi ndoto zangu, ikiwa ni kweli nyinyi mnajua tafsiri za ndoto na mnaweza kuzitolea fatwa .
Mfalme alipowauliza alitumia neno : “Ikiwa” , kwa maana alijua kuwa hii ndoto ni ngumu kuiagua/kuitafsiri.
Na kweli walishindwa kujua tafsiri ya ndoto hii na wakadai kuwa hii ndoto si ndoto iliyosafika bali ni fikra na mawazo ya mchana tu kwa hiyo haina maana.
Allah -aliyetukuka -alitaka kumnyanyua Yusufu na kudhihirisha ubora wake akakadiria kuwa mfalme awaite wale wajuzi waliopo kwake ili wamtafsirie ndoto hiyo kabla ya kuitwa Yusufu -amani iwe juu yake -na pindi waliposhindwa akalipeleka jambo hilo kwa Yusufu na hapo ndipo kulipodhihiri ubora wa Yusufu -amani iwe juu yake -kwa sababu lau angempelekea Yusufu moja kwa moja kusingedhihiri ubora wa Yusufu -amani iwe juu yake.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tatu 19, 1443H ≈ Jul 18, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•