MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU -AMANI IWE JUU YAKE-. Makala namba (24)

قال تعالى :

Amesema (Allah) aliyetukuka-:

قَالَ لَا يَأْتِيكُمَا طَعَامٌ تُرْزَقَانِهِ إِلَّا نَبَّأْتُكُمَا بِتَأْوِيلِهِ قَبْلَ أَن يَأْتِيَكُمَا ۚ ذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِي رَبِّي ۚ إِنِّي تَرَكْتُ مِلَّةَ قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ

(Yusufu) akasema: Hakitakujieni chakula chochote mtachoruzukiwa ila nitakwambieni tafsiri yake kabla hakijakujieni. Haya ni katika yale aliyonifundisha Mola wangu mlezi. Hakika mimi sifuati mila ya watu wasiomuamini Allah, na wakawa hawaiamini Akhera . (37)

Maelezo ya muandaaji:

Mazungumzo baina ya Yusufu -amani iwe juu yake- na wale vijana aliowakuta gerezani yaliendelea, Yusufu-Amani iwe juu yake- akawaambia kuwa kutokana na Utume aliopewa anaweza kuwafasiria ndoto zao na mambo mengine yaliyofichikana .

Akawaambia : Hakitakujieni chakula usingizini isipokuwa nitawatafsiria hiki chakula na kuwafafanulia au maana yake:

Hakitakujieni chakula mukiwa macho isipokuwa nitawaeleza aina ya hiki chakula na asili yake kama vile ulivyokuwa muujiza wa nabii Isa- Amani iwe juu yake- pale alipowaambia watu wake katika suratul-Aali Imran:

وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ ۚ

Na nitakwambieni mtakavyovila na mtakavyoweka akiba katika nyumba zenu. (49)

Kisha Yusufu -Amani iwe juu yake- akawaambia:

“Haya ni katika yale aliyonifundisha Mola wangu Mlezi”.

Yusufu -Amani iwe juu yake- aliwaambia hivi ili wasimdhanie kuwa yeye ni kuhani au mchawi, na pia aliwaambia maneno haya ili kuiweka tauhidi karibu na wao na ifahamike kwa wepesi kwao .

Kisha Yusuf akawaekeza kuwa yeye hafuati dini ya watu wasiomuamini Allah na siku ya mwisho ,na hii ni dalili kuwa kuamini siku ya mwisho ni jambo ambal lipo na limetajwa katika vitabu vya Manabi waliopita kinyume na wanavyosema watu wa Falsaf kuwa kuamini siku ya mwisho kumetajwa na Muhammad pekee katika Quran.

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 26, 1443H ≈ December 1, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *