Mazingatio katika kisa cha nabii Yusufu-amani iwe juu yake-. Makala namba (25)

Makala namba (25) .

قال تعالى :

Amesema (Allah) aliyetukuka-:

{ وَٱتَّبَعْتُ مِلَّةَ ءَابَآءِىٓ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْحَٰقَ وَيَعْقُوبَ ۚ مَا كَانَ لَنَآ أَن نُّشْرِكَ بِٱللَّهِ مِن شَىْءٍۢ ۚ ذَٰلِكَ مِن فَضْلِ ٱللَّهِ عَلَيْنَا وَعَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ}

“Na nimefuata Mila ya baba zangu Ibrahimu na Is-haqa na Yaqubu. Hatuna haki ya kumshirikisha Allah na chochote. Hiyo ni katika fadhila za Allah zilizo juu yetu na juu ya watu (wengine) ; lakini watu wengi hawashukuru” (38) .

Maelezo ya muandaaji:

Kisha Yusuf- amani iwe juu yake- akawaambia kuwa yeye amefuata na kushikamana na dini ya babu zake Ibrahimu na Is-haqa na ya baba yake Yaqubu ,kisha akawaeleza kuwa si haki kwao na haiwi kwao na hawawezi kumshirikisha Allah kwa sababu wao wote familia yao ni familia ya utume ,kama alivyosema Allah-aliyetukuka pindi alipokuwa akiwaelezea Malaika waliokuja kwa Ibrahimu-amani iwe juu yake- :

ۖ رَحْمَتُ ٱللَّهِ وَبَرَكَٰتُهُۥ عَلَيْكُمْ أَهْلَ ٱلْبَيْتِ ۚ إِنَّهُۥ حَمِيدٌ مَّجِيدٌ

“ Rehema za Allah na Baraka zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika yeye (Allah) ni mwenye kusifiwa na kutukuzwa ”

Suratul- Hud 73 .

Kisha akasema:

“Hiyo ni katika fadhila za Allah zilizo juu yetu” .

Hii ni dalili kuwa fadhila kubwa zaidi ni neema ya dini, neema ya uislamu,neema ya tauhidi, neema ya kumuabudia Allah pekee.

Kisha akasema:

“Na juu watu (wengine)” .

Kwa maana hii dini ni fadhila kubwa kutoka kwa Allah kwa wale watu walioiamini hii dini .

“lakini watu wengi hawashukuru” .

Watu wengi walipojiwa na dini hii hawakushukuru kwa maana hawakumuabudia Allah kwa kushukuru neema ya kumpwekesha Allah na imani .

Tanbih: Hapa tumeona Yusufu-amani iwe juu yake- amewaita babu zake kuwa ni baba zake kwa maana babu ana nafasi ya baba, kama vile mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- alipomuelezea mjukuu wake Al-Hasan -Allah amridhie- alimuita kwa sifa ya kuwa ni mwanaye akasema:

إِنَّ ابْنِي هَذَا سَيِّدٌ وَإِنِّي أَرْجُو أَنْ يُصْلِحَ اللَّهُ بِهِ بَيْنَ فِئَتَيْنِ مِنْ أُمَّتِي

“ Bila shaka mwanangu huyu ni mtukufu, na bila shaka mimi nataraji Allah atapatanisha baina ya makundi mawili katika umati wangu kwa kupitia yeye ” .

البخاري .

Kama ikiwa ni hivyo yaani babu ana nafasi ya baba na ndiyo maana katika madhehebu (ya Kishafii) katika daraja za mawalii, wa kwanza ni baba mzazi na kama hayupo au hastahiki anayefuata ni babu wa binti ambaye ni baba mzazi wa baba wa binti, na hapa utaona ujinga waliokuwa nao baadhi ya mababu ambao huwatania wajukuu zao wa kike kuwa ni wachumba wao au wake zao na wajukuu wa kike kuwatania babu zao kuwa ni waume zao, jambo hili halifai na ni ujinga wa hali ya juu huu!

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 27, 1443H ≈ December 2, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *