https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU- AMANI IWE JUU YAKE .
Makala namba (16) :
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka- :
وَلَقَدْ هَمَّتْ بِهِۦ ۖ وَهَمَّ بِهَا لَوْلَآ أَن رَّءَا بُرْهَٰنَ رَبِّهِۦ ۚ كَذَٰلِكَ لِنَصْرِفَ عَنْهُ ٱلسُّوٓءَ وَٱلْفَحْشَآءَ ۚ إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُخْلَصِينَ
Na yule mwanamke akamkazia nia ya kufanya naye machafu ,na (Yusuf) nafsi yake ilipitiwa na mawazo ya kukubali .Lau si yeye kuona dalili za Mola wake Mlezi (zenye kumkemea kufanya hilo ) .Tumefanya namna hivi ili tumwepushie kila jambo la ubaya na la uovu (kama kuzini) .Hakika yeye alikuwa katika waja wetu waliosafishwa .
سورة يوسف ٢٤
Maelezo ya muandaaji:
Kuna kauli nyingi mno za wanachuoni katika kuitafsiri aya hii lakini tarjama niliyoitoa hapo ni kulingana na tafsiri ya baadhi ya wanachuoni kama vile ibn ‘Atwiyyah -Allah amrahamu- na katika wanachuoni wa zama hizi ni Ibn ‘Uthaimin- Allah amrahamu- kwa maana yule mwanamke alimkazia nabii Yusuf nia ya kufanya naye machafu na alijitahidi kwa vitendo kutaka kulifanya hilo,ama Yusuf – amani iwe juu yake-alipitiwa na mawazo ya kukubali kisha yakatoweka kwa sababu ya yale yaliyopo katika moyo wake kama vile imani ,elimu,kheri na Allah akamuepusha na hili, na faida tunayoipata pale Allah-aliyetukuka- aliposema :
ۚ إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُخْلَصِينَ
.Hakika yeye (Yusufu) alikuwa katika waja wetu waliosafishwa .
Na katika kisomo kingine :
ۚ ٱلْمُخْلِصِينَ
Maana yake : Waliomtakasia Allah ibada ,na Allah akawasafisha, na hii ni dalili kuwa Tauhid ni sababu – kwa idhini ya Allah- ya kuokoka na madhambi .Na bila shaka tauhidi ni sababu ya kuokoka duniani na kaburini pindi mtu atapoulizwa maswali : Ni nani Muabudiwa wako,ni ipi dini yako, ni nani Mtume wako ? , maswali haya hatoyajibu isipokuwa mtu wa tauhidi aliyepewa taufiki na Allah na hiyo ndiyo sababu ya kuokoka kwake na pia ni sababu ya kuokoka akhera /siku ya kiama .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 19, 1442H ≈ June 29, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•