Mbona munaibomoa nyumba mutakayohamia !

◾️ قال ابن القيم رحمه الله :
Amesema ibn l-Qayyim-Allah amrahamu-:

“أكثر أصحاب القبور معذبين، والفائز منهم قليل،

Wengi zaidi katika watu wa makaburini ni wenye kuadhibiwa ,na mwenye kufaulu miongoni mwao ni wachache,

فظواهر القبور تراب، وبواطنها حسرات وعذاب،

basi juu ya makaburi (unaona) udongo ,na ndani yake ni majuto na adhabu,

ظواهرها بالتراب والحجارة المنقوشة مبنيّات، وفي باطنها الدواهي والبِليَّات.

Nje yake ni udongo na mawe yaliyonakshiwa, hali yamejengewa ,na ndani yake ni misiba na mabalaa.

تغلي بالحسرات كما تغلي القدور بما فيها، ويحقّ لها وقد حيل بينها وبين شهواتها وأمانيها.

Hutokota kwa majuto, kama vitokotavyo vyungu kwa vile vilivyomo ndani yake na yanahaki ya huko (kutokota) ,na hakika kumewekwa kizuizi baina yao (hao maiti) na baina ya matamanio yao na matarajio yao .

تالله لقد وعظَتْ فما تركتْ لواعظ مقالاً،

Wallah !hakika (makaburi) yametoa mawaidha na hayakuacha (hata) neno kwa mtoa mawaidha ,

ونادت: يا عمّار الدنيا لقد أعمرتم داراً موشكة بكم زوالاً،
Na (makaburi) yameita : Enyi wenye kuijenga dunia ,bila shaka mumeijenga nyuma inayokaribia kukuondokeni ,

وخرّبتم داراً أنتم مسرعون إليها انتقالاً،

Na mumeibomoa nyumba ambayo nyinyi munaiendea kwa haraka ,

عمّرتم بيوتا لغيركم منافعها وسكناها،

Mumezijenga nyumba zisizokuwa zenu manufaa yake na kuishi kwake ,

وخربتم بيوتاً ليس لكم مساكن سواها”.

Na mumezibomoa nyumba (ambazo) nyinyi hamuna makazi isipokuwa hayo .

📚📚 الروح (١ / ١٢٩).

Maelezo ya mfasiri:

Bila shaka lau tungezuru makaburi kwa mazingatio basi hilo pekee linatosha kuwa ni mawaidha yenye kulainisha nyoyo kama alivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:

” زُوْرُوْا الْقُبُوْرَ فإنَّها تذَكِّرُكُمُ الْآخِرَةَ “

“ Zuruni makaburi hakika huko (kuzuru) kunakumbusha akhera”

رواه ابن ماجه وغيره .

Bila shaka kutembelea makaburi kunakumbusha akhera, kunakumbusha kifo na hilo litamsukuma mtu kufanya matendo mema yatakayoijenga nyumba yake ya akhera ambayo hujengwa kwa matendo mema.

Lakini wengi tumeghafilika na safari hii ya akhera, ndiyo maana tunatilia umuhimu kuiimarisha dunia na hali sisi tutaiacha karibuni na tunaibomoa nyumba ya ahera ambayo tunaielekea tena kwa haraka ,kwa sababu kila siku mpya inayoingia kwetu basi inatusogeza karibu na makaburi yetu kama alivyosema Al-hasan Al-Basry – Allah amrahamu-:

يا ابن آدم ..
إنّما أنتَ أيام ، فإذا ذهبَ يومٌ ذهبَ بعضك .

Ewe binadamu, hakika si vingine wewe ni masiku (tu) na siku inapoondoka basi huondoka baadhi ya (umri wako) .

•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 9 , 1445H =Apr 18, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *