كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله- عبر حسابه على تويتر .
Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim- Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :
النَّاس شجرةٌ أصلها: آدم عليه السَّلام، وفروعها: أبناؤه، وأوراقها: الأُمم،
Watu ni (kama) mti, shina lake ni Adamu -amani iwe juu yake- ,na matawi yake ni wanaye ,na majani yake ni nyumati,
وثمارها النَّافعة: المؤمنون، فهم شرف شجرة الآدميَّة، ومعيار منزلتها الحقيقيَّة،
Na matunda yake yenye manufaa ni (waislamu) waumini basi hao (waumini) ndiyo utukufu wa mti wa kibinadamu na ni kipimo cha daraja lake la kweli ,
ومن لم يكن مؤمنًا فهو من حطب النَّار.
Na yule asiyekuwa muumini basi huyu ni kuni za moto (wa Jahanam).
Ameandika tarehe 6,Mfungo tano /1444 H sawa na tarehe 2, Sep 2022M
Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amuhifadhi-amewafananisha wanadamu na mti ambao shina lake ndiyo baba yetu Adamu-amani iwe juu yake- na matawi ya mti huo ni wanaye na majani yake ndiyo sisi wanadamu ambao tumegawanyika mataifa mbalimbali kama vile Waarabu ,waafrika,wazungu, n.k , na matunda yenye manufaa ya mti huo ni waumini kwa maana wale wenye kumpwekesha Allah, na hao waumini ndiyo utukufu wa mti huo wa kibinadamu na ndicho kipimo cha daraja lake la kweli ,na bila shaka muumini ni mtukufu na daraja lake limenyanyuliwa mbele ya Allah, na yeyote asiyekuwa muumini basi mtu huyo makazi yake ni motoni ,kama alivyosema Allah -aliyetukuka-:
وَأَمَّا الْقَاسِطُونَ فَكَانُوا لِجَهَنَّمَ حَطَبًا .
“ Na wanaokengeuka hao watakuwa kuni za Jahanamu ”
سورة الجن ١٥
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 13, 1443H ≈ Sep 9, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•