Makala namba (2) .
◾️ سُـئلـت اللّجنة الدائمة للإفتاء
برئاسة الشَّــيخُ العلّامــة/
عـبدُ الـعَزِيـز بن بـاز -رحمهُ الله –
Iliulizwa kamati ya kudumu ya kutoa fatwa chini ya uongozi wa mwanachuoni mkubwa Abdul-Aziz bin Baz -Allah amrahamu –
مـا هـي آداب تـلاوة الـقـرآن الـكـريـم ؟
Ni zipi adabu za kusoma qurani tukufu?
❪✵❫ الجَـــ☟ـــوَابُ:
Jawabu :
【 لـتـلاوة الـقـرآن آداب مـنهـا】
Kusoma qurani kuna adabu katika hizo (ni) :
(❹) يـستحسن أن يـجلس عـند قـراءة الـقرآن عـلى هـيئة حـسنة ولـباس حـسن مـستقبل الـقبلة ،
وفـي مـكان مـحترم يـليق بالـقرآن .
Ni suna pindi anaposoma qurani aketi mkao mzuri na (avae) mavazi mazuri (aketi) hali ya kuelekea qibla na katika sehemu yenye kuheshimika inayonasibiana na quran.
(❺) يـستحب أن يـقرأ بـخضوع وخـشوع وتـمهل وتـدبر وتـفكر فـي آيـاته ، ومـنصرف بـقلبه وحـواسه لـما يـقرأ مـن الـقرآن ، ولا يـقطع الـقراءة بـكلام الآدمـيين مـن غـير حـاجة .
Inapendeza asome kwa unyenyekevu na utulivu wa viungo ,kwa upole na kuzingatia na kufikiria katika aya zake na aupeleke moyo wake na viungo vyake kwa kile anachokisoma katika quran na wala asikate kisomo kwa Sababu ya kuzungumza na wanadamu bila ya haja.
📓📙 الفتوى رقم 【 ١٨٦٧٦ 】
Maelezo ya mfasiri :
Adabu ya nne (4) :
Ni kuisoma qurani kwa adabu zilizotajwa hapo na kufanya hivi ni katika kukitukuza kitabu cha Allah na hivi ndivyo walivyokuwa wema waliopita mfano:
كان أبو العالية الرياحي – رحمه الله –
Alikuwa Abuu Al-‘aliyah Arriyahiy -Allah amrahamu –
إذا قرأ اعتمّ، لبس عمامة، وارتدى ثيابه، واستقبل القبلة.
Pindi anaposoma qurani huzungusha kilemba kichwani (yaani) huvaa kilemba na huvaa nguo yake (mzuri) na huelekea (upande wa) kiblah .
تفسير القرطبي (٢٧/١).
Kwa hiyo unapotaka kusoma qurani vaa nguo yako mzuri paka manukato unukie, na tafuta sehemu mzuri yenye utulivu wala usisome qurani sehemu ambayo inapigwa mziki au yanafanyika maovu, na kaa mkao mzuri hali ya kuelekea kibla kwa sababu ni suna kuelekea kibla katika vikao mbalimbali na haswa vikao vya ibada, na ubora huu umethibiti katika kauli yake Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:
«إِنَّ لِكُلِّ شَيْءٍ شَرَفاً، وَإِنَّ شَرَفَ الْمَجَالِسِ مَا اسْتُقْبِلَ بِهِ الْقِبْلَةُ»
Hakika kila kitu kina kitukufu chake, na hakika kikao kitukufu ni kile (kikao) kilichoelekezwa kiblah.
رواه الطبراني في الكبير عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عنهُ.
Adabu ya tano (5) :
Aisome qurani kwa mazingatio na unyenyekevu na kufikiria maana za aya kama alivyosema Allah -aliyetukuka -:
كِتَٰبٌ أَنزَلْنَٰهُ إِلَيْكَ مُبَٰرَكٌ لِّيَدَّبَّرُوٓاْ ءَايَٰتِهِۦ وَلِيَتَذَكَّرَ أُوْلُواْ ٱلْأَلْبَٰبِ
(Na hiki) Kitabu; tumekiteremsha kwako,chenye baraka nyingi ;ili wapate kuzizingatia Aya zake,na ili wenye akili wawaidhike.
ص ٢٩
Hii ni dalili kuwa wenye kuisoma qurani na wakazifiria aya zake na kuzizingatia na wakawaidhika nayo basi hao ndiyo wenye akili yaani akili ya uongofu na bila shaka kusudio kubwa la kuteremshwa qurani ni kuwaidhika nayo.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shabani 6, 1443H ≈ Mar 9, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•