Makala namba (3)
◾️ سُـئلـت اللّجنة الدائمة للإفتاء
برئاسة الشَّــيخُ العلّامــة/
عـبدُ الـعَزِيـز بن بـاز -رحمهُ الله –
Iliulizwa kamati ya kudumu ya kutoa fatwa chini ya uongozi wa mwanachuoni mkubwa Abdul-Aziz bin Baz -Allah amrahamu –
مـا هـي آداب تـلاوة الـقـرآن الـكـريـم ؟
Ni zipi adabu za kusoma qurani tukufu?
❪✵❫ الجَـــ☟ـــوَابُ:
Jawabu :
【 لـتـلاوة الـقـرآن آداب مـنهـا】
Kusoma qurani kuna adabu katika hizo (ni) :
(❻) يـستحب أن يـرتل الـقرآن بـصوت حـسن مـع تـبيين الـحروف والـحركات والـعناية بـأحكام الـتجويد حـسب قـدرته .
6- Ni suna aisome quran kwa utaratibu na kwa sauti mzuri pamoja na kuzibainisha herufi na haraka na kutilia umuhimu hukumu za taj-widi kadri ya uwezo wake.
(❼) إذا كـان أحـد يـسمعه وهـو يـقرأ الـقرآن أو يـصلي ، فـينبغي أن لا يـزعجهم بـرفع الـصوت أو يـشوش عـلى مـن يـصلي .
7- Kukiwa kuna yeyote anayemsikia na hali huyo (mtu pia) anasoma quran au anaswali basi inatakikana asiwashughulishe (watu) hao kwa kunyanyua sauti au kumchanganya yule anayeswali.
📓📙 الفتوى رقم 【 ١٨٦٧٦ 】.
Maelezo ya mfasiri :
Adabu ya ya sita katika adabu za kusoma qurani ni kuwa msomaji anatakiwa aisome qurani kwa utaratibu, na kwa sauti mzuri, na kwa kuziweka wazi herufi kama kaaf,alifu n.k na pia kuziweka wazi haraka kama dhwammah ,fat’hah n.k ,na pia atilie umuhimu hukumu za taj-wid, kwa sababu Allah -aliyetukuka-amemuamrisha Mtume wake -swala na salamu za Allah zimfikie- aisome Qur’an kwa uzuri na upole na kuzingatia pale aliposema:
وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا
Na soma Qur’an kwa utaratibu /kwa utungo .
المزمل ٤
Na vile vile Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- amehimiza kuisoma qurani kwa sauti mzuri pale aliposema:
زيِّنوا القُرآنَ بأصواتِكم
Kipambeni (kisomo cha) Qur’an kwa sauti zenu .
صحيح ابن حبان | الصفحة أو الرقم : ٧٤٩
Na adabu ya saba ni kuwa mtu anapokuwa anasoma Qur’an na kukawa na mtu au watu wanaomsikia na hali hao watu pia wanasoma Qur’an au wanaswali basi anatakiwa asinyanyue sauti katika kusoma kwake qurani kwa sababu hilo litapelekea kuwachanganya hao wenzake wanaosoma Qur’an au wanaoswali na imethibiti hadithi kuwa siku moja Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- alikuwa amekaa itikafu msikitini akawasikia Maswahaba wakinyanyua sauti zao kwa kusoma Qur’an na hali Mtume akiwa katika jengo lake la itikafu basi akafungua panzia na akasema:
ألا إنَّ كلَّكم مُناجٍ ربَّه ، فلا يُؤذِينَّ بعضُكم بعضًا ، ولا يرفعَنَّ بعضُكم على بعضٍ بالقراءةِ . أو قال : في الصلاةِ
Sikilizeni hakika nyote (nyinyi kila mmoja) ana mnong’oneza Mola wake,basi baadhi yenu wasiwaudhi baadhi na wala baadhi yenu wasinyanyue sauti juu ya baadhi kwa kusoma (Qur’an). Au alisema katika swala.
أخرجه أحمد (11915)، والنسائي في ((السنن الكبرى)) (8092) باختلاف يسير.
Ufafanuzi:
Ni haramu kunyanyua sauti kwa kusoma Qur’ani likiwa hilo litamchanganya mtu anayeswali kwa maana ikithibiti kuwa hiyo sauti inawaudhi na kuwachanganya basi itakuwa ni haramu ,na kama hiyo sauti haiwachanganyi na kuwaudhi basi jambo hilo linachukiza.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shabani 7, 1443H ≈ Mar 10, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•