Makala namba (4)
◾️ سُـئلـت اللّجنة الدائمة للإفتاء
برئاسة الشَّــيخُ العلّامــة/
عـبدُ الـعَزِيـز بن بـاز -رحمهُ الله –
Iliulizwa kamati ya kudumu ya kutoa fatwa chini ya uongozi wa mwanachuoni mkubwa Abdul-Aziz bin Baz -Allah amrahamu –
مـا هـي آداب تـلاوة الـقـرآن الـكـريـم ؟
Ni zipi adabu za kusoma qurani tukufu?
❪✵❫ الجَـــ☟ـــوَابُ:
Jawabu :
【 لـتـلاوة الـقـرآن آداب مـنهـا】
Kusoma qurani kuna adabu katika hizo (ni) :
(❽) لا يـهذ الـقارئ الـقرآن هـذًّا فـلا يُـفهم عـنه مـا يـقول ، ولا يـمططه ويـمده مـدًّا يـخل بـألفاظه فـيخرجه عـن الـمقصود مـن تـلاوته ، بـل وسـطًا بـين ذلـك .
8- Msomaji Qur’ani asiisome haraka haraka hii Qur’an (akawa) hakifahamu kile anachokisema na wala asizirefushe (herufi) na kuvuta (herufi) uvutaji unaoharibu (maana ya) matamko yake akaitoa katika makusudio yake ya kuisoma, bali (aisome) katinakati baina ya hivyo.
(❾) لا يـقرأ الـقرآن بـألحان الـغناء ، كـألحان أهـل الـفسق ، ولا بـترجيع الـنصارى ولا نـوح الـرهبانية ، فـإن ذلـك كـله لا يـجوز .
9- Na wala asiisome Qur’an kwa sauti za miziki,kama sauti za waovu na wala (asisome) kwa sauti za Manaswara na wala (kwa) vilio vya watawa na hakika yote hayo hayafai
📓📙 الفتوى رقم 【 ١٨٦٧٦ 】.
Maelezo ya mfasiri:
Adabu ya nane katika adabu za kusoma Qurani ni msomaji kuisoma Qur’an polepole bila ya kuharakisha kwa sababu akisoma kwa haraka itampelekea asizingatie maana yake, na wala asivute herufi za kuvuta kupita kiasi na wala asizikate ,na kuna nasaha alizozitoa ibn Masud -Allah amridhie kuhusu hili pale aliposema:
لاَ تَنْثِرُوهُ نَثْرَ الدَّقْلِ وَلاَ تَهُذوهُ هَذ الشِّعْرِ، قِفُوا عِنْدَ عَجَائِبِهِ، وَحَرِّكُوا بِهِ الْقُلُوبَ، وَلاَ يَكُونُ هَمُّ أَحَدِكُمْ آخِرَ السُّورَة
Musiitawanye hiyo (Qurani) utawanyaji wa tende zilizochakaa na wala musiisome kwa haraka (kama) yanavyosomwa kwa haraka mashairi ,simameni katika maajabu yake na zitinginisheni (nyoyo) kwa hiyo (Qur’an) na wala yasiwe makusudio ya mmoja wenu (kufika) mwisho wa sura .
أخرجه ابن أبي شيبة في المصنف (٨٧٣٣).
Ufafanuzi:
Hapa ibn Masud -Allah amridhie- anatutahadharisha kuwa tusisome Qur’an kwa haraka ikawa inasikika sauti lakini haifahamiki maana yake kama vile tende zilizochakaa na kukauka pindi zinaposambazwa hutoa sauti za kugongana gongana , na vile vile tusisome Qur’an kwa haraka kama washairi wanaposoma mashairi yao ambao malengo yao ni kusifiwa kwa ufasaha na uhodari waliokuwa nao na wala hawazingatii kile wanachokisoma .
Na akatuamrisha pindi tunaposoma Qur’an tuzingatie maana yake na maajabu yaliyomo ndani na maana mbalimbali na uongofu ,na vilevile nyoyo zetu zitingishike kama zinavyotingishika ndimi zetu pindi tunaposoma kitabu cha Allah ,na wala isiwe pupa ya msomaji ni kumaliza sehemu aliyoikusudia kuisoma kwa haraka bila ya kuzingatia bali asome kwa kuzingatia na kuifanyia kazi.
Adabu ya tisa ni mtu kutoisoma Qur’an kwa sauti za miziki, au sauti za Manaswara au sauti za vilio vya watawa wao kufanya hivyo ni haramu
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shabani 9, 1443H ≈ Mar 12, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•