Makala namba (1)
◾️ سُـئلـت اللّجنة الدائمة للإفتاء
برئاسة الشَّــيخُ العلّامــة/
عـبدُ الـعَزِيـز بن بـاز -رحمهُ الله –
Ili ulizwa kamati ya kudumu ya kutoa fatwa chini ya uongozi wa mwanachuoni mkubwa Abdul-Aziz bin Baz -Allah amrahamu –
مـا هـي آداب تـلاوة الـقـرآن الـكـريـم ؟
Ni zipi adabu za kusoma qurani tukufu?
❪✵❫ الجَـــ☟ـــوَابُ:
Jawabu :
【 لـتـلاوة الـقـرآن آداب مـنهـا】
Kusoma qurani kuna adabu katika hizo (ni) :
(❶) أن يـكون قـارئ الـقرآن عـمله خـالصًا لـوجه الله ، لا ريـاء ولا سـمعة ، ولا يـطلب بـه أجـرة ؛ لأن عـبادته تـقربًا إلـى الله .
1- Awe msomaji qurani matendo yake ni kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah, si kwa kujionesha na wala si kwakutaka kusikika ,na wala asitake ujira kwa huko (kusoma qurani) kwa sababu ibada yake ni kwa ajili ya kujiweka karibu na Allah.
(❷) مـن آداب تـلاوة الـقرآن أن يـستعيذ بـالله مـن الـشيطان الـرجيم عـند ابـتدائه للـقراءة ، ويـقرأ بـسم الله الـرحمن الـرحيم إذا كـان ابـتداء قـراءته مـن أول الـسورة عـدا سـورة الـتوبة .
2- Miongoni mwa adabu za kusoma qurani ni (msomaji) ajikinge kwa Allah kutokana na Shetani aliyefukuzwa katika rehema za Allah wakati wa kuanza kwake kusoma ,na atasoma “kwa jina la Allah mwingi wa rehema mwenye kurehemu ” ikiwa mwanzo wa kusoma kwake ni mwanzoni mwa sura isipokuwa suratu ttaubah.
(❸) يـستحب لـقارئ الـقرآن عـند قـراءته أن يـكون عـلى وضـوء ، فـإن كـانت قـراءته مـن مـصحف وجـب عـليه الـوضوء ؛ لـقوله ﷺ :
«لا يمس القرآن إلا طاهر» .
3- Ni suna kwa msomaji wa qurani wakati wa kusoma kwake awe na udhu ,na kukiwa kusoma kwake ni kutoka msahafuni ni wajibu juu yake achukue udhu kwa kauli yake-swala na salamu za Allah zimfikie- :
“Asiiguse qurani ila aliyekuwa twahara “
📓📙 الفتوى رقم 【 ١٨٦٧٦ 】.
Maelezo ya mfasiri :
Hizi ni miongoni mwa adabu za kusoma qurani ambazo wamezitaja wanavyuoni hawa na idadi yake ni kumi na moja (11) ,na tatu za mwanzo ni hizi :
1- Aitakase nia yake pindi anaposoma qurani kwa maana asome kwa ajili ya kutaka thawabu na radhi za Allah na bila shaka neema kubwa kabisa peponi ni kuuona uso wa Allah -mtukufu .
2- Na anapoanza kusoma qurani ajikinge kwa Allah na shetani aseme hivi :
(أعوذ بالله من الشيطان الرجيم)
(Najikinga kwa Allah kutokana na Shetani aliyefukuzwa katika rehema za Allah) .
Na anapoanza mwanzo wa sura asome :
بِسْمِ اللهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيْمِ
(Kwa jina la Allah mwingi wa rehema na mwenye kurehemu) .
Isipokuwa mwanzo wa suratu ttaubah asianze na Bismillah..
3- Ni suna anaposoma qurani awe na udhu kwa yule anayesoma bila ya kushika msahafu au akatumia msahafu wa mtandaoni, ama yule atakayeshika msahafu huyo ni lazima achukue udhu kwa sababu ni haramu kuishika qurani bila ya udhu.
Inaendelea -Allah akitaka.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shabani 5, 1443H ≈ Mar 8, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•