Mfululizo wa adabu za kusoma Qurani tukufu.

Makala namba (5) :

◾️ سُـئلـت اللّجنة الدائمة للإفتاء
برئاسة الشَّــيخُ العلّامــة/
عـبدُ الـعَزِيـز بن بـاز -رحمهُ الله –

Iliulizwa kamati ya kudumu ya kutoa fatwa chini ya uongozi wa mwanachuoni mkubwa Abdul-Aziz bin Baz -Allah amrahamu –

مـا هـي آداب تـلاوة الـقـرآن الـكـريـم ؟

Ni zipi adabu za kusoma qurani tukufu?

❪✵❫ الجَـــ☟ـــوَابُ:
Jawabu :

【 لـتـلاوة الـقـرآن آداب مـنهـا】

Kusoma qurani kuna adabu katika hizo (ni) :

❿)- ومـن آداب الـقراءة أن يـمسك عـن القراءة إذا تـثاءب حـتى يـذهب الـتثاؤب ؛ تـعظيمًا لله ؛ لأنـه مـخاطب ومـناج لـربه ، والـتثاؤب مـن الـشيطان .

10 – Na katika adabu za kusoma (Qur’an msomaji) ajizuie na kusoma pindi atakapo piga miayo mpaka imuondoke miayo kwa kumtukuza Allah kwa sababu huyo (msomaji) ni mwenye kumsemesha na Kumng’oneza Mola wake mlezi na kupiga miayo kunatokana na Shetani.

11-【ومـن آداب الـقراءة أن يـقف عـند آيـة الـرحمة فـيسأل الله مـن فـضله ، وأن يـقف عـند آيـة الـعذاب والـوعيد فـيستجير بـالله مـنه ، وعـند آيـة الـتسبيح فـيسبح ، وذلـك فـي غـير الـصلاة الـمفروضة】

11- Na katika adabu za kusoma (Qurani) ni msomaji kusimama wakati wa aya ya rahmah na amuombe Allah katika fadhila zake na asimame wakati wa aya ya adhabu na makemeo na ajikinge kwa Allah kutokana na hiyo (adhabu) ,na wakati wa aya ya tasbih alete tasbih ,na hilo (asilifanye) katika swala za faradhi.

📓📙 الفتوى رقم 【 ١٨٦٧٦ 】.

Maelezo ya mwandishi:

Adabu ya kumi katika adabu za kusoma Qur’an ni msomaji ajizuie kusoma pindi anapopiga miayo mpaka amalize kupiga miayo kwa sababu kufanya kwake hivyo ni kumtukuza Allah kwani msomaji Qur’an anamsemesha Mola wake Mlezi na ana mnong’oneza na kupiga miayo kunatokana na Shetani ,kama alivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:

«التَّثَاؤُبُ مِنَ الشَّيْطَانِ، … ».

“ Kupiga miayo kunatokana na Shetani…”

البخاري

Kupiga miayo ni alama ya kuchoka na Shetani huipenda hali hii kwa muumini na pia mtu anatakiwa aache kusoma Qur’an anapokuwa na usingizi mpaka akawa unasinzia anatakiwa aache kusoma Qur’an kwa muda huo kwa sababu anaweza akachanganya herufi au akakosea kusoma au aya zikachanganyika, au akataja herufi isiyokuwepo kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie:

” إذا قام أحدكم من الليل، فاستعجم القرآن على لسانه، فلم يدر ما يقول، فليضطجع“

Pindi mmoja wenu atakaposimama usiku Qur’an ikawa ngumu ulimini mwake (akawa) hajui kile anachokisema,basi alale”

رواه مسلم وغيره

Adabu ya kumi na moja na ya mwisho katika adabu walizozitaja hawa wanavyuoni ni adabu ya msomaji Qur’an kusimama pindi anaposoma aya inayotaja rahma za Allah na amuombe Allah katika rehma zake na fadhila zake, na pia aya ya adhabu ajikinge na adhabu zake, na aya ya iliyotaja tasbih yaani kumtakasa Allah anatakiwa amtakase Allah, na huu ndiyo mwenendo wa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -kama anavyosema Hudhaifah bin l-Yaman akielezea kisomo cha Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – :

كان إذا مرَّ بآيةِ خوفٍ تعوَّذَ ، و إذا مرَّ بآيةِ رَحمةٍ سألَ ، و إذا مرَّ بآيةٍ فيها تَنزيهُ اللهِ سبَّحَ

Alikuwa pindi anapopita aya ya hofu (adhabu) hujikinga, na anapopita aya ya rehma huomba, na anapopita aya ndani yake kuna kumtakasa Allah humtakasa.

صحيح الجامع | الصفحة أو الرقم : ٤٧٨٢
Mwisho :

Msomaji Qur’an anapokuwa nje ya swala ni suna kwake kufanya hivyo moja kwa moja kwa maana hakuna tofauti ya wanavyuoni katika hilo, ama akiwa ndani ya swala wanavyuoni wametofautiana na wanachuoni hawa wameitia nguvu kauli ya ibn Qudam katika Mahanabilah kwa maana atafanya hivyo katika swala ya suna si faradhi, ama madhehebu yetu ya kishafii ni suna katika swala zote za faradhi na za suna kama anavyosema Annawawiy :

قال الشافعي وأصحابنا: يسن للقارئ في الصلاة وخارجها إذا مر بآية رحمة أن يسأل الله تعالى الرحمة…
Amesema Shafiy na watu wetu : Ni sunnah kwa anayesoma Qur’an ndani ya swala na nje yake pindi anapopita aya ya rahmah amuombe Allah rehma …

ويستحب ذلك للإمام والمأموم والمنفرد…

Na ni suna (kufanya) hivyo kwa imamu na maamuma na anayeswali peke yake …

لأنه دعاء فاستووا فيه كالتأمين.

Kwa sababu hiyo ni dua wakalingana wote kama vile kuitikia aamiin

ثم قال: وقال بمذهبنا جمهور العلماء من السلف ممن بعدهم.

Kisha akasema (Annawawiy) : Na wanachuoni wengi zaidi wanameshika madhehebu yetu katika (wale wema) waliopita na wale waliokuja baada yao.

المجموع: ٦٦/٤

Mwandishi : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shabani 12, 1443H ≈ Mar 15, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *