Mfululizo wa hukumu za maiti. (No.3)

السؤال:

Swali: 🎤

هل صحيح أنه إذا أدخل المؤمن القبر تأتيه حورية ينقطع عقدها فينظم هذا العقد حتى تقوم الساعة؟

Je, ni sahihi kwamba muumini anapoingizwa kaburini humjia msichana mrembo (wa peponi na) hukatika kidani chake, Basi (huyu muumin) hukiunganisha hiki kidani mpaka kiama kitakapo simama?

الجواب:

Jawabu: 📚

هذا ليس بصحيح،الصحيح أن الإنسان إذا دخل في قبره،

(Kauli) hii sio sahihi,

Sahihi ni kwamba mwanadamu atakapo ingizwa katika kaburi lake,

وسأله الملكان،وأجاب بالصواب

Na malaika wawili wakamuuliza (maswali),

Na akapatia kujibu (maswali),

فسح له في قبره مد البصر،

Basi hupanuliwa (hukunjuliwa) kaburini lake (mpaka likawa) upeo wa macho yake,

وأتاه من روح الجنة ونعيمها،

Na humjia raha zake /na upepo wake mwanana wa peponi na neema zake,

ويأتيه عمله الصالح في أحسن صورة ويبقى عنده.

Na humjia matendo yake mema katika sura nzuri mno na hubakia kwake.

📚 مجموع فتاوى ابن عثيمين (17/443)

Maelezo ya mfasiri:

Usahihi ni huu alioutaja sheikh-Allah amrahamu- kuwa mtu anapozikwa hujiwa na Malaika wawili ambao katika baadhi ya riwaya yametajwa majina yao : منكر و نكير

Munkar na Nakir, Malaika hawa sifa zao zimetajwa kuwa : Nyuso zao ni nyeusi na macho yao ni ya bluu, watamuuliza mwanadamu maswali matatu:

1- Ni nani muabudiwa wako?

2- Ni ipi dini yako?

3- Ni yupi mtume wako?

Na haya maswali ndio mtihani na majaribio atakayopewa mwanadamu kaburini ndiyo maana Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie amesema:

” إنَّ هذِهِ الأمَّةَ ستُبتَلَى في قبورها “

” Hakika huu uma utajaribiwa katika makaburi yao ” .

Muumini atajibu maswali haya na ataneemeshwa kaburini mwake kwa neema mbalimbali kama alivyoeleza sheikh hapo juu , ama kafiri au mnafiki atatahayari na atapigwa na nyundo ya chuma na atapiga ukelele atakaosikiwa na kila kiumbe ila wanadamu na majini.

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 14, 1443H ≈ Dec 18, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *