Mfululizo wa makala kuhusiana na masuala ya biashara; Makala ya tisa [9]

https://t.me/fawaidussalafiyatz

MFULULIZO WA MAKALA ZINAZOHUSIANA NA MASUALA YA BIASHARA!

MAKALA NAMBA 09;

SHARTI ZA BIASHARA YA KUTANGULIZA THAMANI NA KUCHUKUA BIDHAA BAADAE.

السادس: أن يقبض الثمن في مجلس العقد.

6 – (Sharti) ya sita: (Muuzaji anatakiwa) apokee thamani (ya bidhaa) katika kikao cha kuuziana.

فتاوى اللجنة الدائمة – المجموعة الأولى . باب السلم (١٤/٩٣)

Maelezo:

Hii ni sharti ya sita katika sharti ya biashara ya salam yaani biashara ya kutanguliza thamani na bidhaa kuchukua baadae, nayo ni: Anatakiwa mnunuzi atoe thamani (pesa) yote na kumkabidhi muuzaji katika kikao cha biashara yaani pale pale mahali walipozungumza kuhusu biashara hii na wakakubaliana. Na hilo ni kwa sababu kama mnunuzi hakumkabidhi muuzaji thamani (pesa) yote katika kikao cha kuuziana biashara hiyo itakuwa ni kuuziana deni kwa deni nayo ni haramu na batili. Na kuuziana deni kwa deni hapa ni kuwa bidhaa haipo na pia thamani ya bidhaa hiyo haipo, kwa maana muuzaji anadaiwa na mnunuzi anadaiwa! na ubaya wa uuzaji huu yaani deni kwa deni mara nyingi hupelekea katika riba au huwa ni katika kamari yaani pata potea au mtu hufaidika na kile ambacho hajakimiliki.

ITAENDELEA.. Usikose makala namba 10 in shaa Allah.

Muandaaji: fawaidusalafiya.net. Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Sha’aban 12, 1442H ≈ March 25, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *