KITABU CHA PILI :
4 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .
س رقم: ٤
Swali no.4:
مَا هِيَ الْعِبَادَةُ ؟
Ibada ni nini ?
ج:
Jawabu:
الْعِبَادَةُ هِيَ: كُلُّ مَا يُحِبُّهُ اللّٰهُ ، وَ يَرْضَاهُ مِنَ الْأَقْوَالِ، وَ الْأَعْمَالِ ،الظَّاهِرَةِ والْبَاطِنَةِ.
Ibada ni : Kila analolipenda Allah na analoliridhia katika kauli na matendo yanayodhihiri na yaliyojificha .
سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]
Maelezo ya mfasiri:
Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :
Mwanangu jana nilikueleza kuwa lengo la kuumbwa kwetu ni kumuabudia Allah -aliyetukuka- bila ya kumshirikisha na chochote,ikiwa ni hivyo ni lazima ujue maana ya ibada ili umuabudie Allah kwa elimu ,na ibada maana yake ni hii :
“ Ni kila analolipenda Allah na kuliridhia katika maneno na matendo yanayodhihiri na yaliyojificha /ya moyoni ”.
Hapa mwanangu utaona kuwa kuna ibada ambazo zinadhihiri katika viungo vyetu ima kwa ndimi zetu kwa kuzitamka , au kwa viungo vingine kwa kuzitenda ,na pia kuna ibada zisizodhihiri hizi ni ibada za moyoni,hebu sasa ngoja tutoe mifano wa kila ibada hizo :
1- Ibada za kimazungumzo:
Miongoni mwa ibada zinazodhihiri kwa kuzitamka ni dhikri/nyiradi na nyiradi bora zaidi ni Kusoma quran, na pia kuamrisha mema na kukataza mabaya ,n.k
2- Ibada za kimatendo ni nyingi pia katika hizo ni : Kuswali, Kutoa zaka, Kutoa sadaka,n.k
3-Ibada za matendo ya moyo nazo ni kama vile: kuogopa ,kutegemea ,kutaraji, kujikinga n.k , na ibada hizi za matendo ya moyo ni ibada bora zaidi kuliko hizo ibada zinazodhihiri .
Usikose makala namba 5 inayofuata in shaa Allah
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 16, 1444H ≈ Dec 10, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•