KITABU CHA PILI :
5 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .
س رقم: ٥
Swali no. 5 :
مَا هِيَ أَمْثِلَةُ الْعِبَادَةِ الْقَلْبِيَّةِ ؟
Ni ipi hiyo mifano ya ibada za kimoyo ?
ج:
Jawabu:
مِنْ أَمْثِلَتِهَا الْخَوْفُ، وَ الرَّجَاءُ ،والتَّوَكُّلُ ،والْمَحَبَّةُ.
Miongoni mwa mifano yake (ni) : Hofu, na kutaraji, na kutegemea, na kupenda .
سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]
Maelezo ya mfasiri:
Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :
Mwanangu jana tulisoma maana ya ibada na tukatoa baadhi ya mifano ya ibada kutokana na umuhimu wa ibada na ndiyo lengo la kuumbwa kwetu leo tutaendelea na ufafanuzi wa ibada, na tunaanza na ibada za matendo ya moyo kwa sababu hizi ni ibada bora zaidi, na kama nilivyokueleza ibada hizi zipo nyingi mno,na miongoni mwa hizo ni hizi tulizozitaja hapo juu :
Hofu :
Makusudio ya hofu ambayo ni ibada ni kumuogopa Allah ,na hofu hii inajulikana pia kwa jina la hofu ya siri nayo ni ile hofu iliyoambatana na mapenzi kwa Allah na kutukuza na kujidhalilisha kwake .
Kutaraji:
Kutamani katika kitu ambacho hakuna anayekimiliki isipokuwa Allah na huku ni kutaraji kuliko kusanya kujidhalilisha na kunyenyekea .
Kutegemea:
Ni mja kudhihirisha udhaifu wake kwa Allah na kumtegemea yeye.
Kupenda :
Mapenzi ya kumpenda Allah ambayo ni ibada ni yale mapenzi yanayoambatana na kumyenyekea na kumtukuza .
Mwanangu fahamu kuwa aina zote hizi nne za ibada na nyinginezo haifai kufanyiwa asiyekuwa Allah -aliyetukuka-na mwenye kuzipeleka kwa asiyekuwa Allah mtu huyo atakuwa ameingia katika ushirikina .
Usikose makala namba 6 inayofuata in shaa Allah
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 18, 1444H ≈ Dec 12, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•