KITABU CHA PILI :
6 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .
س رقم: ٦
Swali no.6:
مَا هِيَ أَمْثِلَةُ الْعِبَادَةِ الْقَوْلِيَّةِ ؟
Ni ipi hiyo mifano ya ibada za kimaneno ?
ج:
Jawabu:
مِنْ أَمْثِلَتِهَا : الدُّعَاءُ ، وَ الْاسْتِغَاثَةُ، وَ الْاسْتِعَانَةُ، وَ النَّذْرُ .
Miongoni mwa mifano yake (ni):
Dua , na kutaka msaada wa kuokolewa wakati wa shida,na kutaka msaada katika kufikia kile unachokikusudia ,na kuweka nadhiri .
سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]
Maelezo ya mfasiri:
Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :
Mwanangu somo lililopita tulisoma aina za ibada za matendo ya moyo na ufafanuzi wake , na leo tujifunze aina za ibada za kimaneno/ kikauli ,na kwa leo tutazifafanua hizo aina nne zilizotajwa hapo juu :
Dua :
Dua imegawanyika sehemu mbili kuna dua ya ibada kwa maana ibada zote tunazozifanya ni dua kwa sababu malengo yetu ya kufanya ibada ni kumuomba Allah atulipe na kutuingiza peponi .
Na aina ya pili ya dua ni dua ya masuala ina maana kule kumuomba kwetu Allah maombi mbalimbali kunazingatiwa kuwa ni ibada.
Kutaka msaada wa kuokolewa :
Mtu kumtaka Allah msaada wa kuokolewa pindi anapopatwa na shida mbayo hakuna anayeweza kuiondoa isipokuwa yeye Allah tu basi hiyo ni ibada .
Kutaka msaada:
Kumtaka msaada Allah katika yale ambayo hakuna anayeyaweza isipokuwa yeye Allah hiyo ni ibada .
Nadhiri:
Kuweka nadhiri ni ibada na nadhiri inayokusudiwa hapa ni mtu kuiwajibishia nafsi yake kufanya ibada maalumu ya sunnah kwa ajili ya Allah bila ya kuifunga hiyo ibada na chochote mfano akasema:
” Najiwajibishia kufunga siku tatu kwa ajili ya Allah ”.
Mwanangu kama nilivyokueleza katika somo lililopita kuwa ibada hizi na nyinginezo haifai kupelekewa yeyote isipokuwa Allah ,na mwenye kuzipeleka kwa asiyekuwa Allah -aliyetukuka-atakuwa ameingia katika ushirikina .
Usikose makala namba 7 inayofuata in shaa Allah
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 19, 1444H ≈ Dec 13, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•