Mfululizo wa makala za vikadi vya aqidah(itikadi) kwa watoto wa kiislamu.

KITABU CHA PILI :

3 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .

س رقم: 3
Swali no.3:

مَا هُوَ الْأَمْرُ الَّذِي خَلَقَنَا اللّٰهُ مِنْ أَجْلِهِ ؟

Ni jambo lipi ambalo Allah ametuumba kwa ajili ya hilo ?

ج:
Jawabu:

خَلَقَنَا اللّٰهُ لِعِبَادَتِهِ وَحْدَهُ لَا شَرِيْكَ لَهُ .

Ametuumba kwa ajili ya kumuabudia yeye pekee asiyekuwa na mshirika.

سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.

[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amhifadhi]

Maelezo ya mfasiri:

Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kuwa :

Lengo kuu la kuumbwa kwake ni kumuabudia Allah -aliyetukuka-pekee na yote anayoyafanya hapa duniani ni nyenzo tu za kulifikia lengo kuu ambalo ni kumuabudia Allah pekee bila ya kumshirikisha na chochote, hata chakula unachokula ,nyumba unayoijenga,kazi unayoifanya ili upate riziki yote haya ukiyafanya kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah yanakuwa ni ibada .

Mfano kama ukila kwa lengo la kushiba ili upate nguvu ya kufanya ibada basi huku kula kwako ni ibada, hata baba yako anapotatafuta riziki ili ailishe familia yenu kwa kutaraji thawabu kutoka kwa Allah basi huku kufanya kwake kazi ni ibada , na pia hata ukivaa nguo mpya /mzuri kwa lengo la kudhihirisha neema za Allah kwa kumshukuru basi tendo hilo ni ibada, kwa hiyo tambua mwanangu kuwa lengo la kuumbwa kwetu na kuwepo kwetu hapa duniani ni kumuabudia Allah kwa kumpwekesha , kama nilivyokueleza jana na nikanukuu kauli yake Allah -aliyetukuka -pale aliposema :

{ وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ }

{ Sikuwaumba majini na wanadamu ila wapate kuniabudu}

الذاريات: ٥٦

Kwa hiyo mwanangu tambua kuwa kila jambo unalolifanya ambalo ni njia au nyenzo ya kuifanya ibada fulani basi jambo hilo pia linapewa hukumu ya ibada kama nilivyokueleza.

Usikose makala namba 4 inayofuata in shaa Allah

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 19, 1444H ≈ Dec 9, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *