KITABU CHA PILI :
7- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .
س رقم: ٧
Swali no.7:
مَا هِيَ أَمْثِلَةُ الْعِبَادَةِ الْفِعْلِيَّةِ ؟
Ni ipi hiyo mifano ya ibada za kimatendo ?
ج:
Jawabu:
مِنْ أَمْثِلَتِهَا : الذَّبْحُ ، والصَّلَاةُ .
Miongoni mwa mifano yake (ni) :
Kuchinja na kuswali .
سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]
Maelezo ya mfasiri:
Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :
Mwanangu somo la jana lilikuwa linahusiana na ibada za kimaneno na ufafanuzi wake , leo pia tutaendelea kusoma aina za ibada lakini leo tutasoma ibada za kimatendo nazo pia zipo aina nyingi sana lakini kwa leo tutazifafanua hizi aina mbili zilizotajwa hapo juu :
Kuchinja:
Makusudio ya kuchinja hapa ni kuchinja kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allah-aliyetukuka-.
Swala:
Swala mwanangu ni ibada bora zaidi inayofanywa na viungo, na swala ni jambo la kwanza litakalohesabiwa siku ya Kiama katika yale yanayohusiana na haki za Allah, na swala alifaradhishiwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- akiwa mbinguni usiku wa safari ya Mi’iraji na hili linajulisha umuhimu na nafasi ya kipekee ya ibada hii, kwa hiyo mwanangu simamisha swala ndani ya wakati wake .
Mwanangu kama ninavyokueleza kila siku kuwa ibada zote zinawajibika kupelekwa kwa Allah -aliyetukuka- na mwenye kuzipeleka kwa asiyekuwa Allah basi ameingia katika ushirikina mfano :Yule anayemchinjia jini,au mizimu n.k yote haya ni katika matendo ya kishirikina .
Usikose makala namba 8 inayofuata in shaa Allah
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 21, 1444H ≈ Dec 15, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•