KITABU CHA PILI :
8- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .
س رقم: ٨
Swali no.8 :
مَا هِيَ شُرُوْطُ صِحَّةِ قَبُوْلِ الْعِبَادَةِ ؟
Ni zipi sharti za kusihi kukubaliwa ibada ?
ج:
Jawabu:
لَهَا شَرْطَانِ هُمَا:
إِخْلَاصُ الْعِبَادَةِ لِلّٰهِ، وَ مُتَابَعَةُ رَسُوْلِ اللّٰهِ- صَلَّى اللّٰهُ عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ- فِيْهَا .
(Ibada) ina sharti mbili nazo ni:
1- Kumtakasia ibada Allah, aliyetukuka.
2- Na kumfuata Mtume wa Allah -swala na salamu za Allah zimfikie-katika hiyo (ibada) .
سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]
Maelezo ya mfasiri:
Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia:
Mwanangu fahamu kuwa ibada yoyote haikubaliwi na Allah ila iwe imetimiza sharti mbili nazo ni :
1- (Ikhlaswi) kwa maana ibada ifanywe kwa ajili ya Allah tu ,ama mwenye kufanya ibada kwa kumkusudia asiyekuwa Allah ibada yake hiyo si yenye kukubaliwa hata kama ibada hiyo itakuwa imethibiti katika sheria, na mfanyaji atapata madhambi .
2- Kumfuata Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-, kwa maana ibada hiyo anayoifanya ni lazima iwe imethibiti katika yale yaliyokuja katika sheria au inarudi katika misingi ya sheria na kanuni zake ,na mwenye kufanya ibada ambayo haipo katika sheria basi hatolipwa katika ibada yake hiyo bali atapata madhambi, na hata kama ataifanya kwa kumtakasia Allah yaani kwa ikhlaswi .
Mwanangu zingatia sharti hizi mbili za ibada na usifanye amali yoyote ya kiibada ambayo haikukusanya sharti hizi mbili .
Usikose makala namba 9 inayofuata in shaa Allah
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 23, 1444H ≈ Dec 17, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•