Mfululizo wa makala za vikadi vya itikadi kwa watoto wa kiislamu .

KITABU CHA PILI :

10 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .

س رقم: ١٠
Swali no. 10

مَا هُوَ الْإِسْلَامُ ؟

Uislamu ni nini ?

ج:
Jawabu:

هُوَ الْاسْتِسْلَامُ لِلّٰهِ بالتَّوْحِيْدِ ، والْانْقِيَادُ لَهُ بالطَّاعَةِ، والْبَرَاءَةُ مِنَ الشِّرْكِ وَ أَهْلِهِ .

Ni kujisalimisha kwa Allah kwa kumpwekesha, na kumnyenyekea kwa kutii, na kujiweka mbali na ushirikina na watu wake .

سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.

[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]

Maelezo ya mfasiri:

Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :

Mwanangu hii ndiyo maana ya Uislamu kwa ujumla kwa maana hii ndiyo dini ya Mitume wote-amani iwe juu yao-na vile vile neno “Uislamu” hapa lina maana maalumu ya dini aliyotumwa nayo Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- ambayo imekusanya itikadi na sheria .

Mwanangu fahamu kuwa : Uislamu wa mtu hautimii mpaka mtu ajitenge na ushirikina na watu wake/washirikina kwa maana unatakiwa uuchukie ushirikina na washirikina na hii ndiyo maana ya asili ya neno kujitenga mbali na ushirikina na washirikina .

,mwanangu tambua kuwa yeyote ambaye hauchukii ushirikina /ukafiri na watu wake mtu huyo si muislamu, na hata kama anaupenda uislamu na waislamu.

mwanangu fahamu kuwa haifai kuwapenda washirikina na makafiri kwa sababu za kidunia na kufanya hivyo ni upungufu wa imani kama vile wale wanaowapenda wachezaji mbalimbali wa mpira ambao ni makafiri, au akawapenda makafiri kwa sababu ya maendeleo makubwa waliyokuwa nayo kidunia ,n.k ,haya yote ni katika madhambi makubwa yenye kupelekea upungufu wa imani ama akiwapenda kwa sababu ya dini yao basi huyo atakuwa amekufuru kama wao .

Mwanangu tunaposema kuwa tunauchukia ushirikina na watu wake ,haina maana kuwa hatuamiliani na makafiri katika miamala ya kidunia bali tunaamiliana nao katika miamala ya kidunia na pia tunawafanyia wema lakini bila ya kuwapenda .

Usikose makala namba 11 inayofuata in shaa Allah

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 27, 1444H ≈ Dec 21, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈• ✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *