KITABU CHA PILI :
12 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .
س رقم: ١٢
Swali no.12 :
مَا مَعْنَى لَا إِلٰهَ إِلَّا اللّٰهُ ؟
Ipi maana ya ” hakuna aabudiwaye isipokuwa Allah ” ?
ج:
Jawabu:
مَعْنَاهَا : لَا مَعْبُوْدَ بِحَقٍّ إِلَّا اللّٰهُ .
Maana yake: Hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Allah .
سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]
Maelezo ya mfasiri:
Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :
Mwanangu tunaposema :
” Hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Allah” ina maana vinavyoabudiwa ni vingi mno kwa maana miungu ya upotevu ni mingi mno ,kuna watu wanaabudia masanamu,watu
wema,mizimu ,makaburi,na kuna wale wanaoabudia Mitume kama vile Manaswara ambao wanamuabudia Masih Isa mwana wa Mariam-amani iwe juu yake-lakini miungu yote hii si miungu ya haki, anayeabudiwa kwa haki ni Allah-aliyetukuka- pekee ,yeye ndiye aabudiwaye kwa haki.
Mwanangu hiyo ndiyo maana sahihi ya tamko hili la tauhidi ama wale wanaotafsiri kwa kusema :
” Hakuna aabudiwaye isipokuwa Allah “,
tafsiri hii si sahihi na inaleta maana mbaya yenye kuashiria kuwa kila kinachoabudiwa ni Allah na hii ni itikadi ya kikafiri inayojulikana kwa jina la “Wahdatul-wujud” .
Usikose makala namba 13 inayofuata in shaa Allah
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 3, 1444H ≈ Dec 27, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•