Mfululizo wa makala za vikadi vya itikadi kwa watoto wa kiislamu

KITABU CHA PILI :

2 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .

س رقم: ٢

Swali no.2:

مَا هُوَ أَوَّلُ وَاجِبٍ عَلَى الْعَبْدِ ؟

Ni upi wajibu wa mwanzo juu ya mja ?

ج:
Jawabu:

أَوَّلُ وَاجِبٍ عَلَى الْعَبْدِ هُوَ : مَعْرِفَةُ اللّٰهِ بالتَّوْحِيْدِ .

Wajibu wa mwanzo juu ya mja ni kumtambua Allah kwa kumpwekesha .

سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.

[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amhifadhi]

Maelezo ya Mfasiri:

Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto kuwa: Jambo la kwanza linalowajibika juu ya mja ni kutambua kuwa yeye ameumbwa na Allah -aliyetukuka-na lengo la kuumbwa na Allah ni kumpwekesha yeye yaani kumuabudia Allah pekee bila ya kumshirikisha na chochote kama alivyosema Allah -aliyetukuka-katika Qurani :

{ وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ }

{ Sikuwaumba majini na wanadanamu ila wapate kuniabudu }

الذاريات: ٥٦

Aya hii inajulisha kuwa majini na wanadamu wameumbwa ili wamuabudie Allah na kama wameumbwa ili wamuabudie Allah basi watakuwa wameamrishwa kumuabudia Allah ,na ibada iliyokokotezwa na tukufu zaidi ni tauhidi kwa maana kumpwekesha Allah ,na neno ibada linapotajwa katika Quran bila ya kufungwa lina maana ya tauhid yaani kumpwekesha Allah kwa kumuabudia peke yake bila ya kumshirikisha na chochote .

Usikose makala namba 3 inayofuata in shaa Allah

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 13, 1444H ≈ Dec 7, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *