MFULULIZO WA MAKALA ZINAZOHUSIANA NA MASUALA YA BIASHARA.

MAKALA NAMBA 01;

KATIKA AINA ZA BIASHARA ZILIZOHARAMISHWA NA ZIMEENEA SANA HATA KATIKA MITANDAO!

NI MTU KUUZA ASICHOKIMILIKI!

Katika biashara zilizoenea katika mitandao ni hii kuna watu wapo hapa Tanzania na wanaweza kuwa na mtaji au hawana mtaji lakini watu hawa wanakuwa na mawakala wao nje ya nchi kama China, huyu wakala anachofanya anaongea na huyo mwenye kumiliki bidhaa kwa maana bosi kisha huyu bosi anamtumia picha ya hii bidhaa huyu wakala na huyu wakala anamtumia picha ya hii bidhaa huyu aliyekuwepo hapa Tanzania na kumwambia bei, Mfano hiyo bidhaa ni shilingi elfu kumi na tano ya Tanzania, kisha yeye huyu huyu wa hapa tanzania anazituma hizi picha za bidhaa katika mitandao mbalimbali na kutangaza kuwa anayehitaji bidhaa hii atume pesa yake ambacho ni kiasi kadhaa, mfano elfu ishirini ya Tanzania ili apate faida ya elfu tano kisha anampa khiyari mteja kuwa anaweza kulipa yote au kiasi fulani na mzigo ukija atachukua, kumbuka kwamba hapa kana kwamba kinauzwa kitu hewa yule wakala mwenyewe hajamiliki na huyu wa hapa Tanzania ndiyo kabisa na tayari amechachukua pesa za watu na huenda ameshakula pesa za watu! tena kwa uhakika yeye hauzi hapa bali ni ujanja fulani tu hapa unatumika! Biashara hii haifai na ni haramu na ushahidi wa hilo ni hadithi ifuatayo:

عَنْ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ رضي الله عنه قَالَ: أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ, فَقُلْتُ: يَأْتِينِي الرَّجُلُ يَسْأَلُنِي مِنْ الْبَيْعِ مَا لَيْسَ عِنْدِي، أَبْتَاعُ لَهُ مِنْ السُّوقِ ثُمَّ أَبِيعُهُ؟ قَالَ: (لَا تَبِعْ مَا لَيْسَ عِنْدَكَ)

Kutoka kwa Hakim bin Hizaam – Allah amridhie – amesema: Nilimwendea mjumbe wa Allah – swala na salamu za Allah zimfikie – na nikasema: (Kuna muda) ananijia mtu ananiomba nimuuzie kile kisichokuwepo kwangu (sikimiliki), Je nimnunulie kutoka sokoni kisha nimuuzie? Akasema (Mtume): { Usiuze kile kisichokuwepo kwako }

رواه الترمذي (١٢٣٢) والنسائي (٤٦١٣) وأبو داود (٣٥٠٣) وابن ماجه (٢١٨٧) وأحمد (١٤٨٨٧). وصححه الألباني في “إرواء الغليل” (١٢٩٢)

Maelezo:

Muamala huu umeenea maeneo mbalimbali utakuta ukienda baadhi ya maeneo ukauliza bidhaa fulani utajibiwa kuwa ipo lakini kwa uhakika hana anachofanya anaelewana bei na mnunuzi kisha mnunuzi anakubali kununua, kisha anaenda kwa jirani yake ananunua ile bidhaa kisha anakuja kumkabidhi huyu mnunuaji! biashara hii haifai na chumo linaloingia ni la haramu.

Ama lau atamwambia mteja sina lakini nisubiri kisha akaenda kwa jirani akanunua kisha akaja akamuuzia muamala huu ni halali kwa maana biashara hii inafaa.

Biashara inayofanana na hii iliyopo katika baadhi ya magroup ya mitandao:

Anatokea mtu katika group la whatsApp anarusha bidhaa fulani kisha anataja na bei na kueleza kuwa mwenye kuhitaji bidhaa hizo basi amtumie pesa, na hali ya kuwa huyu muuzaji hajamiliki hiki anachokiuza na pengine huwenda akatumie ile ile pesa atakayotumiwa kunununulia hizo bidhaa, kwa hiyo muamala huu ni haramu ni katika kuuza kile ambacho muuzaji haja miliki.

Ufafanuzi:

Katazo la kuuza kisichokuwepo kwako linakusanya mambo mawili:

1 – Kuuza kitu kinachomilikiwa na mwingine kabla ya muuzaji kukinunua na kukimiliki yeye mfano ni kama tulioutoa hapo juu.

2 – Aina ya pili ni kuwa mtu anaweza akawa anakimiliki kitu fulani lakini hana uwezo nacho mfano kama vile akauza gari yake iliyokuwa mikononi mwa dhalimu na hawezi kuichukua kwake, hii vile vile haifai.

KWA UFUPI:

Haifai kuuza kitu usichokimilikii, mfano wake ni hizi biashara ambazo watu hurusha picha katika mitandao na kukusanya pesa za watu au kuwauzia au kwa kutoa kiasi cha pesa, biashara hii ni haramu sawa sawa huyu muuzaji akiwa hana mtaji au hata akiwa anamtaji maadamu bidhaa hajaimiliki ni haramu kuiuza anachotakiwa ni kusubiri mpaka bidhaa aimiliki kisha auze.

ITAENDELEA..
Usikose makala namba 02 in shaa Allah.

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Toleo la pili : Mfungo nane 4, 1443H -Dec 8, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *