Kadi namba (4) .
أيها الزوج :
Ewe mume :
الطلاق لا يلجأ إليه الرجل إلا بعد أن يستنفد جميع وسائل الإصلاح الشرعي التي ذكرها الله عز وجل في كتابه والنبي -صلى الله عليه وسلم في سنته في تعامله مع خلافات زوجته.
Mwanamume haikimbilii talaka ila baada ya kumalizika njia zote za kutengeneze za kisheria ambazo amezitaja Allah-aliyeshinda na kutukuka -katika kitabu chake na Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -katika suna zake katika kuamiliana kwake na magonvi ya wake zake
فالطلاق ليس هو الحل الأول لإنهاء المشكلة ؛
Basi talaka si ufumbuzi wa kwanza wa kuondoa tatizo
بل هو آخر الحلول، فمن جعله أول حل كان غير موفق في اختياره
Bali hiyo (talaka) ni ufumbuzi wa mwisho ,basi yule aliyeifanya hiyo (talaka) ni ufumbuzi wa kwanza atakuwa si mwenye kuwafikishwa katika uteuzi wake (huu)
المصدر : الوصية الشرعية للحياة الزوجية ،للشيخ سعيد بن سالم الدرمكي
Maelezo ya mfasiri :
Ewe mume tambua kuwa Allah amekuwekea hatua kadhaa za kutengeneza na kuweka sawa makosa aliyoyafanya mkeo , na hizo hatua ni kama zifuatazo :
1- kumuonya/kumnasihi
2- Kumhama kitandani
3-Kumpiga kidogo kama kule kumuonya na kumhama hakujanufaika.
Amesema Allah-aliyetukuka-:
{ وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا}
{Na ambao mnachelea uasi kwao wanasihini,muwahame katika vitanda na wapigeni. Na kama watakutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Allah ndiye aliye juu na Mkuu.
النساء: ٣٤
Ufafanuzi :
Hizi ndizo hatua za kumkanya mwanamke mjeuri aliyetoka katika twaa ya mumewe :
1- Kumuonya na kumpa nasaha kwa makosa anayoyafanya na kama hili halijasaidia inafuata hatua ya pili
2-Kumhama katika malazi yaani kitandani yaani asilale naye kitandani na kama halijanufaisha hilo basi amhame kwa maneno yaani asimzungumzishe lakini isizidi siku tatu, na kama hatua ya kumhama haijasaidia inafuata hatua ya tatu
3- Kumpiga lakini huku kumpiga kunasharti kadhaa :
(A) : Mtampiga kama dhana yake yenye nguvu inamwambia kuwa akimpiga itakuwa ni sababu ya kuadabika na kuacha huo uasi.
B-Lisiwe pigo lenye kujeruhi
C- Asimpige usoni na sehemu za hatari .
Na bila shaka mwanamke mwema anapofanyiwa hawa hujirekebisha na hurudi katika mstari.
Na kama njia hizo tatu hazijanufaisha basi wapelekwe waamuzi wawili wa upande wa mume na upande wa mke ili wasuluhishe kama alivyoeleza Allah :
وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَٱبْعَثُواْ حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِۦ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَآ إِن يُرِيدَآ إِصْلَٰحًا يُوَفِّقِ ٱللَّهُ بَيْنَهُمَآ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرً
{Na kama mkijua kuwepo mfarakano baina yao (mke na mume) basi pelekeni mwamuzi mmoja kutokana na jamaa za mume, na mwamuzi kutokana na jamaa za mke. Kama wakitaka mapatano Allah atawawezesha.Hakika Allah ni mjuzi Mjuzi wa habari za siri na habari za dhahiri.
النساء ٣٥
Ama kama njia zote hizi hazijanufaisha na mfarakano ukaendelea hapo ndipo mume anaweza kutoa talaka au mke akajivua na lakini wanatakiwa waachane kwa wema.
Inaendelea.. Allah akitaka.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 15, 1443H ≈ Jun 15, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•