Kadi namba (9) .
أختي الزوجة:
(Ewe) dada yangu mke :
تذكري أن الزواج نعمة من الله عليك ، قال- صلى الله عليه وسلم- وهو يخاطب النساء – :
Kumbuka kuwa ndoa ni neema itokayo kwa Allah juu yako ,amesema-swala na salamu za Allah zimfikie -na hali akiwaambia wanawake -:
لعلَّ إحداكنَّ تطولُ أيمتُها من أبويها ، ثم يرزقُها اللهُ زوجَها و يرزقُها منه ولدًا ،
“ Huwenda mmoja wenu ujane wake ukarefuka kwa wazazi wake kisha Allah akamruzuku mume, na akamruzuku mtoto kutoka kwa huyo (mume)”.
السلسلة الصحيحة ٨٢٣ ،
فسمى الزوج رزقا وسمى الولد منه والمال رزقا، والنعمة يحافظ عليها ولا يفرط فيها.
Basi (hapa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -) amemuita mume ni riziki na amemuita mtoto kutoka kwa huyo mume na mali ni riziki, na neema huhifadhiwa na wala hakufanywi uzembe katika hilo.
المصدر : الوصية الشرعية للحياة الزوجية ،للشيخ سعيد بن سالم الدرمكي
Maelezo ya mfasiri:
Baada ya kumaliza kumuusia mume sasa anaanza kumuusia mke kwa usia wake huu wa kumkumbusha kuwa, huwenda huyo mke alikaa muda mrefu kwa wazazi wake bila ya kuolewa kisha akaruzukiwa mume na sheikh -Allah amuhifadhi -akanukuu hadithi ya Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – inayoeleza hayo na katika hadithi hiyo Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -amemuita mume ni riziki ambayo Allah amemruzuku huyo mwanamke, na pia akamuita mtoto aliyempata kutoka kwa huyo mume ni riziki , kwa hiyo mwanamke kuolewa ni neema, na pia kupata mtoto ni neema, na neema inatunzwa na kuchungwa na wala haifai kwa mke kuipoteza neema hii ya kupata mume ,neema ya kuolewa.
Inaendelea.. Allah akitaka.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 10, 1443H ≈ Aug 8, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•