Kadi namba (10) .
أختي الزوجة:
(Ewe) dada yangu mke :
تذكري أن طاعة الزوج من أسباب دخول الجنة ،قال -صلى الله عليه وسلم-:
Kumbuka kuwa kumtii mume ni miongoni mwa sababu za kuingia peponi ,amesema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -:
” إذا صلَّتِ المرأةُ خَمْسَها ، و صامَت شهرَها ، و حصَّنَتْ فرجَها ، وأطاعَت زوجَها ، قيلَ لها : ادخُلي الجنَّةَ مِن أيِّ أبوابِ الجنَّةِ شِئتِ“
“ Atakaposwali mwanamke (swala) zake tano, na akafunga mwezi wake (wa Ramadhani), na akauhifadhi utupu wake, na akamtii mumewe, ataambiwa(siku ya Kiama): Ingia peponi kupitia mlango wowote wa pepo uutakao”
صحيح الترغيب ١٩٣٢ .
وإذا علمت أن الجنة حفت بالمكاره،
Na utakapotambua kuwa pepo imefunikwa na (mambo) yanayochukiza (katika nafsi),
فهذه الأربع تحتاج إلى صبر ومجاهدة نفس لنيل الأجر العظيم وهو الجنة.
Basi haya (mambo) manne yanahitajia subira na kupambana na nafsi ili kupata ujira mkubwa nao ni pepo
المصدر : الوصية الشرعية للحياة الزوجية ،للشيخ سعيد بن سالم الدرمكي
Maelezo ya mfasiri:
Miongoni mwa sababu za mwanamke kuingia peponi ni kumtii mumewe kama alivyoeleza Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -, na pia mke anatakiwa ajue kuwa nafasi ya mume ni kubwa mno kwake, mpaka Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -amesema hivi :
”لَوْ كُنْتُ آمِرًا أَحَدًا أَنْ يَسْجُدَ لِأَحَدٍ لَأَمَرْتُ الْمَرْأَةَ أَنْ تَسْجُدَ لِزَوْجِهَا “
“ Lau ningelikuwa ni mwenye kumuamrisha yeyote kumsujudia yeyote (basi) ningemuamrisha mwanamke amsujudie mumewe ”
رواه الترمذي (١١٥٩)
Ufafanuzi :
Hili ndilo daraja na nafasi ya mume kwa mke kiasi ambacho lau ingefaa kiumbe kumsujudia kiumbe basi mke angeamrishwa kumsujudia mumewe.
Na pia miongoni mwa sababu za mwanamke kuingia peponi ni kuswali swala tano kwa kutimiza sharti zake na nguzo zake, na kufunga mwezi wa Ramadhani kwa maana hata yale madeni anayodaiwa kwa udhuru wa ada yake ya mwezi anawajibika ayalipe ili azingatiwe kuwa amefunga Ramadhani yote, na kuuhifadhi utupu wake kutokana na machafu usipokuwa kwa mumewe.
Inaendelea.. Allah akitaka.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 12, 1443H ≈ Aug 10, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•