Kadi namba (11) .
أيها الزوجة:
Ewe mke :
طلب الطلاق من دون سبب شرعي صحيح من أسباب استحقاق العقوبة يوم القيامة،
Kuomba talaka bila ya sababu ya kisheria sahihi ni miongoni mwa sababu za kustahiki adhabu siku ya Kiama,
قال-صلى الله عليه وسلم-:
Amesema-swala na salamu za Allah zimfikie-:
” أيُّما امرأةٍ سألَتْ زوجَها طلاقَها في غيرِ ما بَأْسٍ ؛ فحرامٌ عليها رائِحَةُ الجنةِ “
“ Mwanamke yeyote aliyemuomba mumewe talaka yake bila ya ubaya wowote (unaompata) basi ni haramu juu yake harufu ya pepo ”
صحيح أبي داود ٢٢٢٦.
وطلب الخلع من غير سبب من علامات النفاق ،
Na kuomba kujivua bila ya sababu ni katika alama ya unafiki ,
قال -صلى الله عليه وسلم-:
Amesema- swala na salamu za Allah zimfikie-:
” المُختلِعات هُنَّ المنافِقاتُ “
“ Wanawake wenye kutaka kujivua (katika ndoa) hao ni wanafiki ”
صحيح الترمذي ١١٨٦
المصدر : الوصية الشرعية للحياة الزوجية ،للشيخ سعيد بن سالم الدرمكي
Maelezo ya mfasiri:
Mke anatakiwa ajiepushe na kuomba talaka bila ya haja na sababu ya kisheria kwa sababu jambo la talaka haliendewi isipokuwa kukiwa na haja inayopelekea hiyo talaka mfano :
Mume akiwa mlevi, au anamtesa mkewe n.k , katika hali kama hizi mke ana haki ya kuomba talaka na wala hana makosa ,ama mwanamke ambaye anaishi na mumewe vizuri na mume akawa anampa haki zake za msingi katika hali hii ni haramu kwa mke kuomba talaka tena yamekuja makemeo makali kutoka kwa Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- kuwa mwanamke mwenye kuomba talaka bila ya sababu ya kisheria basi ni haramu kwake kunusa harufu ya pepo, kwa maana haya ni makemeo makali kutoka kwa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-au ina maana kuwa hatonusa harufu ya pepo kama watakavyonusa wale watakaoingia peponi mara ya kwanza .
Pia ni haramu kwa mwanamke kujivua katika ndoa bila ya sababu ya kisheria na Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-amewafanya wanawake wenye tabia hii ni wanafiki kwa sababu wao hudhihirisha kimuonekano kuwa kilichowapelekea kutaka kujivua ni kuwa wao wanawachukia waume zao na hawawezi kuishi nao lakini si kweli bali makusudio yao ndani ya nyoyo zao ni kuwa wao wanajivua ili wakaolewe na wanaume wengine na kwa ajili hii wakafananishwa na wanafiki kwa sababu wanadhihirisha kinyume na yale yaliyomo katika nyoyo zao .
Kwa hiyo mwanamke haruhusiwi kujivua isipokuwa kukiwa na sababu ya kisheria kama vile ikiwa mwanamke anamchukia mumewe ,au mume anaamiliana naye muamala usiokuwa mzuri kama vile kumtesa na kumnyanyasa.
Inaendelea.. Allah akitaka.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 14, 1443H ≈ Aug 12, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•