https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MIONGONI MWA DUA ZILIZOKUSANYA
قال تعالى:
Amesema (Allah) aliyetukuka:
{ وَقُل رَّبِّ أَدْخِلْنِى مُدْخَلَ صِدْقٍ وَّأَخْرِجْنِى مُخْرَجَ صِدْقٍ وَّٱجْعَل لِّى مِن لَّدُنكَ سُلْطَٰنًا نَّصِيرًا }
Na sema (katika maombi yako) : “Mola wangu !Niingize mwingizo mwema ,na nitoe kutoka kwema .Na unipe hoja iliyowazi inayotoka kwako .”
سورة الإسراء : ٨٠
🔶وهذه الدعوة من أنفع الدعاء للعبد فإنه لايزال داخلا في أمر وخارجًا من أمر فمتى كان دخوله لله وبالله وخروجه كذلك كان قد أدخل مدخل صدق وأخرج مخرج صدق.
Na hii dua ni katika dua zenye manufaa kwa mja ,bila shaka huyo (mja) siku zote ni mwenye kuingia katika jambo (fulani) na mwenye kutoka katika jambo (fulani), na muda ambao kukiwa kuingia kwake ni kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allah ,na kumridhisha Allah ,na kutoka kwake (kukawa) hivyo hivyo bila shaka atakuwa ameingia mwingizo mwema na ametoka kutoka kwema .
المصدر : حادي الأرواح(١ /١٠١)، لابن القيم -رحمه الله-
Maelezo ya muandaaji :
Allah anamuamrisha Mtume wake- swala na salamu za Allah zimfikie- amuombe amuingize mwingizo mwema ,na amtoe kutoka kwema ,na aya hii ni fupi na imekusanya kila sehemu anayoingia muislamu na kutoka inatakikana amuombe Allah amuingize mwingizo mwema na amtoe kutoka kwema , na hilo ni kwa sababu mwanadamu siku zote ima ni mwenye kuingia katika jambo fulani au kazi fulani au ima ni mwenye kutoka , kwa ajili hii inatakikana muislamu amuelekee Allah ,kama Allah alivyomuamrisha Mtume wake – mfano :anapoingia nyumbani na anapotoka, anapoingia katika mji fulani na anapotoka ,anapoingia katika kazi fulani na akatoka , daktari anapoingia chumba cha upasuaji na kutoka , sheikh anapoingia katika muhadhara na anapotoka , kwa maana popote unapoingia sawa sawa iwe ni sehemu au jambo fulani dua hii inaingia ,bila shaka yule ambaye Allah atamuingiza sehemu fulana au katika jambo fulani mwingizo mwema ,na akamtoa kutoka kwema mja huyu atapewa taufiq na Allah na kupatia katika mambo yake na kutakuwa kuingia kwake na kutoka kwake katika maeneo mbalimbali na kazi mbali mbali ni kwa ajili ya kumtii Allah na kutafuta radhi zake .
TANBIH:
Hakuna dalili ya kuihusisha dua hii na muda maalumu au sehemu au idadi maalumu ,bali unaiomba muda wowote na sehemu yoyote
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 5, 1442H ≈ June 15, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•