Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
مما ثبت في فضل يوم عرفة
MIONGONI MWA (HADITHI) ZILIZOTHIBITI KATIKA UBORA WA SIKU YA A’RAFAH
🎙 عن عائشة – رضي الله عنها- أن رسول الله- صلى الله عليه وسلم- قال:
Kutoka kwa mama ‘Aisha -Allah amridhie-kwamba mjumbe wa Allah -swala na salamu zimwendee-amesema:
ما من أيام أكثر من أن يعتق الله فيه عبدا من النار من يوم عرفة, وإنه ليدنو ثم يباهي بهم الملائكة, فيقول: ما أراد هؤلاء؟
“Hakuna katika masiku (ambayo) Allah huwaacha huru na moto waja wengi zaidi kuliko siku ya ‘Arafah, na hakika yeye (Allah) hukaribia kisha hujifakharisha kwa hao (mahujaji) kwa malaika, na (Allah) husema: Wanataka nini hawa?
📚 REJEA:⇣
{أخرجه مسلم}
[ Hadithi Ameipokea Muslim ]
TANBIHI: 🎙
Sifa ya kukaribia ni haki (kweli) kwa namna ambayo inanasibiana na Allah -aliyetukuka- na wala haifai kusema kuwa zinakaribia rehma zake huku ni kupindisha sifa za Allah, na maana ya Allah kujifaharisha kwa Malaika kwa hao mahujaji ni : kuwa Allah huwataja hao mahujaji huko mbinguni kwa Malaika na kuwatukuza
🎙 قال ابن عبد البر- رحمه الله:
AMESEMA IBNU ‘ABDIL – BARR:
(ALLAH AMRAHAMU)
هذا يدل على أنهم مغفور لهم, لأنه لا يباهي بأهل الخطايا إلا بعد التوبة والغفران,والله أعلم.
“Hili linajulisha juu ya kuwa hao (mahujaji) ni wenye kusamehewa na kusitiriwa makosa yao kwa sababu yeye (Allah) hajifakharishi kwa wenye makosa isipokuwa baada ya (kuleta) toba na kusamehewa, na Allah ni mjuzi zaidi .”
📚 REJEA:⇣
{التمهيد لابن عبد البر: ١٢٠/١}
[ Attamhiid,cha ibn ‘Abdil-Barr:1/120
═════════ ❁ ❆ ❁ ═════════
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 9 siku ya arafah, 1442H ≈ 19 ,Jul 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
Nice