يتأكد استحباب صوم شعبان لأمورٍ عظيمةٍ ثلاثة:
Inakokotezwa sunnah ya funga wa mwezi wa shabani kwa sababu ya mambo matatu makubwa:
١) لأن شعبان شهر غفلة،
1) Kwa sababu (mwezi wa) Shabani ni mwezi wa kughafilika,
لكونهِ يقع بين رجب ورمضان،
Kwa kuwa kwake unapatikana baina ya Rajab na Ramadhan,
والعبادة في زمان الغفلة ومكان الغفلة يعظم فضلها.
Na ibada katika muda wa kughafilika na sehemu ya kughafilika ubora wake unakuwa mkubwa.
٢) لأنه شهرٌ ترفع فيه أعمال العباد،
2) Kwa sababu huo (mwezi wa Shabani) ni mwezi ambao hunyanyuliwa matendo ya waja (kwenda kwa Allah),
ومن السُنةِ والخير للعبد أن يُرفع عمله إلى ربه تعالى وهو صائم.
Na katika suna na kheri kwa mja kunyanyuliwa matendo yake kwenda kwa mola wake -aliyetukuka- hali ya kuwa amefunga.
٣) لأنه فعل النبي ﷺ،
3) Kwa sababu hilo ni tendo la mtume – swala na salamu za Allah zimfikie –
وقد كان ﷺ يصوم من شعبان ما لا يصوم من غيره.
Na bila shaka alikuwa – swala na salamu za Allah zimfikie – akifunga (mwezi wa) shabani (ufungaji) ambao hafungi siku nyingine.
📚 من درس (دليل الطالب) (1438/8/1) للشيخ أ.د. سليمان الرحيلي – حفظه الله –
Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi
Muda au kipindi ambacho watu wameghafilika na ibada. Basi ibada inayofanywa kipindi hicho ubora wa ibada unazidi,
Kama vile katika mwezi wa shabani kwa sababu watu wametoka katika mwezi wa Rajab ambao ni katika miezi mitukufu na mwezi unaokuja baada ya Shabani ni Ramadhani,
Kwa hiyo watu hughafilika na ibada katika mwezi shabani kwa kutaraji kuwa Ramadhani inaingia tutakuja kujipinda katk ibada.
Na pia ukiwa katika eneo ambalo ibada fulani watu wameghafilika nayo kuifanya wewe ukawa unaifanya basi tambua kuwa ujira wa ibada hiyo unazidi.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 10, 1443H ≈ Mar 3, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•