MIONGONI MWA MATUNDA NA FAIDA YA KUAMINI QADARI.

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

قال الله تعالى:

Amesema Allah -aliyetukuka:

{وَكَانَ أَمْرُ اللَّهِ قَدَرًا مَّقْدُورًا}

“Na amri ya Allah ni kadari iliyokadiriwa “

سورة فصلت (ص ٤٨)

💡قال العلامة ابن عثيمين -رحمه الله-:

🖊”من ثمرات ‎الإيمان بالقدر، أن الإنسان يكون دائما مطمئنا؛ ليس به قلق، ولا حزن، وإن كان ربما في الصدمة الأولى يجد الإنسان الحزن، لكن بالتصبر، تصبر نفسه”.

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin- Allah amrehemu-:

“Miongoni mwa matunda (faida) za kuamini qadar,ni kwamba Mwanaadamu siku zote anakuwa ni mwenye utulivu ,hana wasiwasi, wala hana huzuni,na hata kama huwenda mtu mwanzoni mwa mtihani akapata huzuni, lakini kwa kujilazimisha na subira nafsi yake husubiri”.

تفسير سورة فصلت (ص ٤٨)

Maelezo:

Kuamini qadar kunakusanya mambo manne :

1- Kuamini kwamba Allah anakijua kila kitu tokea kale/mwanzo usiokuwa na mwanzo .

2- Kuamini kwamba Allah ameandika kila kitu katika ubao uliohifadhiwa

3- Kuamini kwamba yote yanayotokea hayatokei ila kwa kutaka Allah

4- Kuamini kwamba vitu vyote ni viumbe vya Allah.

Na vilevile miongoni mwa faida za kuamini qadar ni:

1- Kumtegemea Allah pekee, pamoja na kuwa kuna sababu unayoitekeleza

2- Mtu kutojivuna wakati anapofanikiwa kwa kupata aliyoyakusudia.

Imepitiwa na: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shawwar/Mfungo tano 15, 1443H ≈ September 22, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *