Miongoni mwa mitihani inayompitia mja duniani

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa:  https://www.fawaidusalafiyatz.net

SIFA ZA MWENYE KUSIFU NA DOSARI ZA MWENYE KUTIA DOSARI !

كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .

Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :

مَدْحُ الْمَادِحِ وَ قَدْحُ الْقَادِحِ ابتلاءٌ يجري على العبد، ونجاته :

Sifa za mwenye kusifu, na dosari za mwenye kutia dosari ni mtihani unaompitia mja , na kuokoka kwake :

ألا يغتر بالمادح ،ولا يُعاق بالقادح ،
Asidanganyike na mwenye kusifu , na wala asizuiliwe na mwenye kutia dosari,

فالاغترار بالمدح يخدش في الإيمان، والوَهَن بالقدح يجرح في الإيقان .

Kuhadaika na sifa kuna parua imani, na (kuwa) dhaifu kwa sababu ya kutiwa dosari kunaijeruhi yakini .

الثلاثاء ١٧ جمادى الآخرة ١٤٤٤ه‍

Maelezo ya mfasiri:

Maneno yenye thamani mno haya kutoka kwa sheikh -Allah amuhifadhi- na ufafanuzi wake ni huu :

Kusifiwa na kupondwa/kutiwa dosari hii ni katika mitihani ambayo mja humpitia hapa duniani na ili apate kuokoka na mtihani huu anatakiwa ashikamane na mambo mawili :

1-Kutohadaika na sifa za wenye kumsifu kwa sababu kuhadaika
na sifa za wenye kusifu hilo linaparua na kutia upungufu imani yake kwa sababu muislamu anatakiwa afanye matendo yake mema kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah na wala si kwa kuwa watu wanamsifu .

2- Ajiepushe na kunyongea kwa sababu ya kutiwa dosari na kusemwa vibawa na watu, kwa sababu kunyongea kunapelekea kupungua yakini ya muislamu katika moyo wake ya kuwa hata kama akitiwa dosari bado ujira wake upo tu mbele ya Allah na wala maneno ya watu hayapunguzi chochote katika thawabu zake .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita   23, 1444H ≈ Oct 8, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *