MIONGONI MWA NJIA ZA KUWAADABISHA WANAWAKE

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

MIONGONI MWA NJIA ZA KUWAADABISHA WANAWAKE !

✍🏻 قال العلامة ابن عثيمين رحمه الله:

👌🏻 ومن تزوج من أجل تأديب زوجته فلا حرج؛
✋🏻لأن بعض النساء لا يؤدبهن إلا النساء،

✅ ولهذا يقال: أدبوا النساء بالنساء.

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn ‘Uthaimin- Allah amridhie- :

Na mwenye kuoa kwa ajili ya kumuadabisha mkewe basi hakuna ubaya (wa hilo),kwa sababu baadhi ya wanawake huadabishwa kwa wanawake,kwa ajili hii husemwa :Waadabisheni wanawake kwa wanawake .

🔥 وكثير من النساء تكون ناشزة لا تؤدي زوجها الحق الواجب له، فيريد أن يريح نفسه وأن يتزوج عليها، وإذا تزوج عليها:

⏪ فمنهن من تستقيم

Na wengi katika wanawake (ktk hao) huwa mgomvi (jeuri) hatekelezi haki za wajibu kwa mumewe ,na (mume) hutaka kuipumzisha nafsi yake ,na kumuolea juu yake (mwanamke mwingine): Basi katika hao (wanawake) kuna wale wanaonyooka

⏪ ومنهن من تزيد نشوزا،
👈🏿✅ وحينئذ يبت طلاقها ويدعها عند أهلها.

👍🏻👍🏻 فالمهم: أن التزوج لتأديب الزوجه الناشز لا بأس به، وأما التزوج لمجارة الناس فلا.

Na katika hao (wanawake) kuna wale wanaozidi ugomvi (jeuri) ,na muda huo ampe talaka yake ya moja kwa moja na akamuache kwa ndugu zake .

Muhimu ni kuwa kuoa kwa ajili ya kumuadabisha mke mgomvi (jeuri) hakuna ubaya ,ama kuoa kwa kuwaiga watu hapana (usifanye)

📚 (اللقاءات الشهرية 503-504/4)

Maelezo:

Kuna baadhi ya wanawake waume zao wanapoongeza mke huzinduka na kuanza kutekeleza haki za mume ,kwa sababu huwa na hofu kuwa huyu mke mpya anaweza kumpiku ndiyo maana hujitahidi kuweza kuitetea nafasi yake ,na hapo ndipo ndoa inakuwa na raha !.
Ama baadhi ya wanawake waume zao wakioa wao huzidi kuleta ugomvi na jeuri ,na hawa dawa yao ni talaka kama hawajirekebisha na madhara yao yakiwa makubwa , lakini sheikh -Allah amrahamu- hakusudii kuwa mtu akioa hatopata misukosuko hapana ,mara nyingi mtu anapoongeza mke hutokea baadhi ya mitihani lakini muhimu ni kusubiri na kuyatatua kwa hekima ,ama ikibidi talaka basi itolewe .

La mwisho alilolisema sheikh -Allah amramu- usioe kwa kufuata mkumbo !fulani ana mathnaa na mimi ngoja niongeze !usifanye hivyo

Na pia mtu anaruhusiwa kuongeza mke kama atatimiza shari za kuongeza nazo ni :

1- Uwezo wa kufanya uadilifu kwa mambo yakidhahiri kama kuwalisha,mavazi,zamu .

2- Uwezo wa kuwahudumia .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 7, 1442H ≈ June 17, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *