Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
شروط الأضحية،
MASHARTI YA (VICHINJWA VYA) UDH’HIYAH
قال العلامة ابن عثيميـن – رحمه الله:
Amesema mwanachuoni mkubwa Ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu:
أن تكون سلـيمة مـن العيوب المانـعة من الإجـزاء،
وهي:
١ – العـوراء: البـيِّن عـورها،
٢ – المـريضة: البيّـن مـرضها،
٣ – العـرجاء: البـيِّن عـرجها،
٤ – العـجفاء: التـي لا تُنـقي ليـس فيـها مُـخ لهـزالها وضـعفها.
(Kichinjwa) kiwe ni chenye kusalimika na aibu/ kasoro zinazozuia kutosheleza (kufaa),
Nazo ni (hizi zifuatazo):
1- Chongo: (ambaye) chongo lake lipo wazi,
2 – mgonjwa: (ambaye) ugonjwa wake upo wazi,
3 – Mwenye kilema: (ambaye) kilema chake kipo wazi,
4 – Aliyekonda: ambaye hana sifa ya kuwa na uroto, (yaani) hana uroto kwa kukonda kwake na udhaifu wake.
📚 المصدر: مـجموع الفـتاوى: (25-12)
[ Chanzo: Maj’muu’u l-fataawaa (12-25) ]
Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi
Maana yake ni kwamba ikiwa mnyama ana aibu na kasoro ambazo zipo wazi, mfano kunaweza kudhihiri maradhi ya mnyama kwa yafuatayo: kama vile ukimshika utahisi ana joto mno linalotokana na maradhi au ukamuona amechokachoka au akawa anakula kidogo na alama nyingine ambazo zinapodhihiri hujulikana kwamba huyu ni mgonjwa ikiwa hakutodhihiri magonjwa itafaa kumchinja lakini inachukiza ama ukimpata ambaye hana aibu na kasoro ni bora zaidi,
Na pia akiwa na aibu na kasoro zaidi ya hizi huyo atakuwa hafai kabisa, mfano akawa kipofu au mwenye maradhi ya ukurutu ambayo huharibu mafuta na nyama ,na yule ambaye hawezi kutembea, pia aliyekatwa makalio yake na, mnyama ambaye amezeeka mpaka akawa hana uroto, hawa hawafai kuchinjwa wa ajili ya udh’hiyah!
Pia kuna aibu ua kasoro zingine ambazo hazipelekei kutofaa kuchinja lakini ni bora zaidi kumpata aliyesalimika nazo, kama vile aliyekatwa sikio au aliyevunjwa pembe, aliyekatwa mkia, au baadhi yake, aliye chanwa sikio lake, aliyekatwa dhakari yake,
ama aliye pondwa korodani zake (aliyehasiwa) huyu inafaa kuchinjwa, tena mara nyingi nyama yake inakuwa mzuri zaidi kwa sababu anakuwa amenona na amenenepa vizuri kwa sababu hatumii nguvu zake katika kumwaga mbegu kwa majike kwa jili hii anakuwa ni mwenye nyama mzuri,
Kwa hiyo kumuhasi mnyama inafaa kwa sababu ya faida ya mlaji na faida yake mnyama mwenyewe nayo ni kunona na kunenepa vizuri ,na pia yule aliye tokwa na meno anafaa kuchinjwa,
Hawa tulio wataja haipendezi mtu kuwa chinja katika udh’hiya, ni vizuri ampate asiyekuwa na aibu na kasoro, huo ndiyo ukamilifu na ndiyo bora zaidi,
Allah amesema:
{ لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ }
(Hamtoufikia wema mpaka mtoe vile mnavyo vipenda).
📁 آل عمران (٩٢)
[ Aal-Imran (92) ]
Tanbihi:
Maelezo haya nimeyatoa na kuyafanyia tarjama kutoka katika sherhe ya bulughul-maraam ya Sheikh Ibn Uthaimin – Allah amrahamu – na nimebadilisha baadhi ya sehemu ili maneno yaafikiane na lugha yetu ya kiswahili.
Uchanganuaji:
Uroto ni yale maji maji yaliyopo katika maungio.
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Iliandaliwa: August 10, 2019M ,ikarudiwa Dhul-Qaadah 28, 1442H ≈ Jul 8, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•