Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
من صفات الزوجة الصالحة:-
MIONGONI MWA SIFA ZA MKE MWEMA:-
الراعية لبيتها
الخادمة لزوجها
MWENYE KUCHUNGA NYUMBA YAKE.
MWENYE KUMTUMIKIA MUME WAKE
قال تعالى :
AMESEMA ALLAH ALIYETUKUKA:
{فالصالحات قانتات حافظات للغيب بما حفظ الله}
{ BASI WANAWAKE WEMA NI WALE WENYE KUDUMU NA WEMA WENYE KUHIFADHI YALE YASIYOONEKANA KWA SABABU ALLAH AMEWAAMRISHA }
[ النساء ٣٤ ,Annisaa 34 ]
قال ابن تيمية – رحمه الله:-
AMESEMA IBN TAIMIYYAH (ALAH AMRAHAMU)
قوله : { فالصالحات قانتات حافظات للغيب بما حفظ الله } يقتضي وجوب طاعتها لزوجها مطلقا من :
KAULI YAKE (ALLAH):
{{ BASI WANAWAKE WEMA NI WALE WENYE KUDUMU NA WEMA ,WENYE KUHIFADHI YALE YASIYOONEKANA (SIRI) KWA SABABU ALLAH AMEWAAMRISHA}}.
(AYA HII) INAPELEKEA UWAJIBU WA MWANAMKE (MKE) WA KUMTII MUME WAKE MOJA KWA MOJA (KAMA VILE):
خدمة، وسفر معه،وتمكين له،وغير ذلك
KUMTUMIKIA,
NA KUSAFIRI NAE,
NA KUMUWEZESHA MUME WAKE KATIKA TENDO LA NDOA ,
NA MENGINEYO YASIYOKUWA HAYO
📚 المصدر: مجموع الفتاوى (٢٦٠/٣٢)
[ Chanzo: Maj’muu’u Al-fataawaa (32/260) ]
MAELEZO YA MFASIRI (ALLAH AMUHIFADHI)
Hizi ni sifa za mke mwema ambazo amezitaja Allah katika kitabu chake ambazo ni:
“Wanawake wema ni wale wenye kudumu na wema na kudumu kumtii Allah”
wanahifadhi siri za nyumba na yale yaliyopo baina yake na mume wake, wanawake wema siku zote ukiwauliza yale yaliyopo baina yake na mume wake husema mazuri hata kama wana lala njaa, Lakini utadhani kuwa wanakula vinono..
Na pia mwanamke mwema huhifadhi utupu wake na mwili wake na mali za mume wake na nyumba yake kwa ujumla hata kama mume hayupo..
kinyume cha hawa ni wanawake waovu ambao si wema na wala hawamtii Allah wala waume zao utawaona wakimueleza siri zao kila mtu!,
tena kuna wengine husimulia mpaka mambo ya unyumba, mambo yale yanayotokea baina ya Mke na mume!
Bila shaka kutoa siri za ndani ya nyumba ni haramu na kutoa siri za tendo la ndoa ni haramu zaidi.
Nina wanasihi wanandoa kuhifadhiana mambo yao katika nyumba zao, na wanawake pia jitahidini kuwa wake wema wenye tabia nzuri na sifa mfano alizo eleza Allah katika kitabu chake kitukufu zilizo elezwa huko juu.
Tunamuomba Allah hifadhi, afya na salama katika ndoa zetu
──────≪✿❒❒✿≫─────
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Tolea la pili :Muharram/Mfungo nne 21, 1443H ≈ August 31, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•