MIONGONI MWA SUNA ZA EID

https://t.me/fawaidussalafiyatz

MIONGONI MWA SUNA ZA SIKUKUU YA EID:

1- Takbira zilizoachwa huru/zi sizofungwa na baada ya swala ,na hizi takbira zinaanza pindi linapozama jua tu siku ya mwisho ya Ramadhani .

2- Ni suna kwa maamuma aende mapema .

3 – Kuoga kwa ajili ya swala ya eid na kupaka manukato .

4- Kujipamba na kuvaa nguo mzuri .

5- Kula tenda kwa idadi ya witri kabla ya kutoka ,kama akisahau hata njiani,au sehemu ya kuswalia eid .

6- Kwenda sehemu ya kuswalia eid kwa miguu.

7- Kwenda kwa njia nyingine na kurudi kwa njia nyingine .

8- Kuswali sehemu za wazi

9- Kutoka wanawake wote wakiwemao vigori ,wenye hedhi ili wakahudhurie mkusanyiko wa waislamu ,na dua zao pamoja na kuwa wenye hedhi hawatoswali .

10- Kupongezana katika eid ni halali kwa maneno na kuombeana dua kama vile ilivyothibiti kwa maswahaba :

” Allah atukubalie sisi na wewe ” .

11- Kudhihirisha furaha ,na kucheza michezo ya furaha ,na kuingiza furaha kwa wengine .

Jiunge nasi

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *