MIONGONI MWA TABIA NJEMA .
قال أبو الوليد الباجي الاندلسي – رحمه الله تعالى -:
Amesema Abuu l-Walid Al-baajiy Al-andalusiy- Allah amrahamu-:
” من حسن الخلق :
Katika tabia njema :
مجاملة الزوجة والأهل ، ومعاشرتهم والتوسعة عليهم
Ni kuamiliana na mke na familia kwa wema na kuchanganyika nao na kuwakunjulia (matumizi)
قال مالك :
Amesema Maliki :
ينبغي للرجل أن يحسن إلى أهل داره حتى يكون أحب الناس إليهم ” اﻫـ .
Inatakikana mtu awafanyie ihsani watu wa nyumbani kwake mpaka awe ni mtu anayependwa zaidi kwao
(المنتقى شرح الموطأ) (٢١٢/٧) .
Maelezo ya mfasiri :
Anasema Abuu l-walid Al-Baaji -Allah amrahamu- kuwa miongoni mwa tabia njema ni mume kuishi vizuri na mkewe na familia na katika kuishi nao kwa wema ni mume kuchanganyika na familia yake na kuwa nao pamoja na kama amebanwa na shughuli basi atenge muda japo kwa wiki mara moja ya kuwa pamoja na familia yake.
Na pia mume anatakiwa aikunjulie familia yake katika matumizi ,kama mume amekunjuliwa riziki basi aikunjulia familia yake katika matumizi kwa kuilisha vyakula vizuri vizuri na vinavyowatosha , na bila shaka ukifanya hivi utakuwa ni mtu anayependwa zaidi katika familia yako kuanzia mkeo na watoto wako .
Amesema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-:
” خيرُكُم خَيرُكُم لأَهْلِهِ وأَنا خيرُكُم لأَهْلي ،..“
“ Mbora wenu zaidi ni yule mbora wenu zaidi kwa wakeze na mimi ni mbora wenu zaidi kwa wake zangu ” .
رواه الترمذي
Ubora hapa unaingia katika upande wa dini kama vile kuwasimamia katika mambo ya ibada, na pia katika upande wa dunia kwa kuishi nao kwa wema kwa kauli na vitendo .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 21, 1443H ≈ Aug 19, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•